Header Ads

DHAMANA YA LULU KUSIKILIZWA JANUARI 25




Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Januari 25 mwaka huu, itasikiliza ombi la kupatiwa dhamana limsanii wa Filamu nchini, Elizabeth Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kuua bila kukusudia Na. 125/2012  msainii mwenzake marehemu Steven Kanumba.

Ombi hilo la dhamana ambalo tayari limeishapangiwa Jaji Zainabu Mruke kuanza kulisikiliza ombi hilo wakati bado kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia bado haijapangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa, limewasilishwa mahakamani hapo  na mawakili wa Lulu ambaye anaishi gereza la Segerea ,na wake Peter Kibatara,Kenned Fungamtama ,Fulgence Massawe.

Kwa mujibu wa hati ya ombi hilo la dhamana,mawakili wa Lulu wameonyesha wamewasilisha ombi lao hilo wameliwasilisha chini ya kifungu cha  148(1) ,(2) Cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002 .
 
“Lulu ni mtu maarufu nchini, anaiomba mahakama hii impatie dhamana na yupo tayari kutimiza masharti ya dhamana yatakayo tajwa na mahakama hii, na anaahidi kuyatimiza masharti hayo wakati akisubiri kesi yake ya msingi ya kuua bila kukusudia itakapopangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa katika mahakama yako tukufu”alidai Wakili Kibatara katika hati hiyo.

Desemba 21 mwaka jana , Hakimu Mkazi Christine Mbando wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu aliifunga kesi ya kuua bila kukusudia Lulu na kuiamishia rasmi kesi hiyo katika Mahakama Kuu, na uamuzi huo wa mahakama ulitokana na upande wa Jamhuri kumsomea maelezo ya kesi yake kwa kina mshtakiwa huyo na kuieleza mahakama kuwa wanakusudia kuleta jumla ya mashahidi tisa.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Januari 22 mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.