MASHAHIDI WAZIDI KUMNYOSHEA VIDOLE SHEIKH PONDA
Na Happiness Katabazi
FUNDI mwashi Hamis Salum Mkangama(30), ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa Oktoba 7 mwaka jana, mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya uchochezi na wizi wa malighahfi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda Issa na
wenzake 49 aliwataka wasimamishe ujenzi wa ukuta wa kutenganisha kiwanja
cha Markas kilichopo Chang’ombe na Msikiti.
Mkangama
ambaye ambaye ni shahidi wa sita wa upande wa jamhuri alitoa madai hayo
jana mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa wakati
akiongwa na wakili Mwanadamizi wa serikali Tumaini Kweka kutoa ushahidi
wake.
Mkangama alieleza kuwa yeye ni fundi mwashi ambaye ambaye anatengeneza matofali na kwamba Oktoba 7 mwaka jana yeye
na wenzie 20 walikuwa katika kiwanja cha Chang’ombe Markas
kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza Ltd akijenga ukuta
unaotenganisha kiwanja cha Chang’ombe Markas na Msikiti na kwamba
walikuwa katika hatua ya kuchimba msingi.
“Ghafla
ilipofika saa 10 jioni alikuja Ponda na akatuuliza nani katuruhusu
tujenge ukuta katika kiwanja hicho, tukamjibu ni Suleiman ambaye ni bosi
wetu, Ponda akatutaka tusimamishe ujenzi haraka kwani eneo hilo bado lina mgogoro ,sisi tukamjibu hatuwezi kusimamisha ujenzi hadi bosi wetu Suleiman aliyetupa kazi hiyo atukataze, sisi tutaendelea na ujenzi:
“Ponda akaamua kuachana na sisi wajenzi akaanza kupiga picha hilo eneo la kiwanja cha Markas ambalo tulikuwa tunajenga ukuta alipomaliza kupiga picha akatoe mlinzi wa eneo lile ambaye alikuwa hamfahamu Ponda wakanza kujibishana na Ponda kisha mlinzi Yule akaamua kumjulisha bosi wake kwa njia ya simu kuhusu ujio wa Ponda na
bosi yule akaja akatutaka tusieendelee na ujenzi
kwani endapo tutaendelea kuna matatizo yanaweza kutokea na akatueleza
kuwa yeye anaenda kuripoti ujio huo wa Ponda katika vyombo vya
dola”alidai Mkangama.
Kwa upande wake Shahidi wa saba, William Milanzi(43) ambaye ni
mlinzi wa eneo linalopakana na kiwanja cha Markas ambapo alidai
amewekwa kufanya kazi hiyo na mtu mmoja aliyemtaja kwa jina la Seif ambaye
ndiye aliyempa jukumu la kulinda pia eneo la Suleiman ambalo ni la
kiwanja cha Markas kwaajili ya kulinda malighafi zilizokuwa zimeifadhiwa
pale ambazo ni matofali, mbao, nondo na malighafi nyingine nyingi.
Milanzi alieleza kuwa Oktoba 12 mwaka jana, alikuwa katika eneo lake la kazi lilopakana na Markas kuanzia asubuhi na kwamba alipoajiriwa alikuwa ameukuta ukuta ambao hivi sasa haupo na kwamba ukuta uliopo sasa ni mpya na kwamba ukuta ule wa zamani ulivunjwa na umati ule uliovamia siku hiyo.
“Ilipofika saa saba mchana ya Oktoba 12 mwaka jana,baada ya Sala ya Ijumaa, niliona umati mkubwa sana na nikaona mbao nilizokuwa nazilinda zikichukuliwa na umati ule na na zikavushwa kupelekwa kwenye kiwancha upande
wa pili wa Markas ….baada ya muda nikaona umati huo unaingia kwenye
mpaka ule uliokuwa uliokuwa ukijengwa kwaajili ya kutenganisha marks na
msikiti na kuanza kuvunja sehemu ndogo iliyokuwa imeezekwa kwa mabati;
“Baada ya kuvunja wakaingia eneo niliokuwa nalinda na kuanza kubeba matofali na kwenda nayo upande wa pili wa eneo la Markas na nilipomjulisha bosi wangu Seif kuhusu hali hiyo, akanitaka niwe mtulivu kwani anafanya mawasiliano na vyombo vya usalama na matofali yale ni mali ya Suleiman”alidai Milanzi.
Aidha
alidai watu toka katika umati ule ambao hakuweza kuwatambua waliwafuata
wao na kuanza tuuliza kama wao ndiyo wenye mali ya kiwanja cha Markas
,akawajibu kuwa wao ni walinzi mwenye mali ni Suleiman na kwamba wale watu sita ambao walikuwa wamefuka vipaza sauti katike eneo hilo walijitambulisha kwao kuwa wao ni waislamu na kwamba wamekuja pale kwaajili ya kuja kuhani eneo lao na
waliwataka walinzi hao wakamweleze bosi wao kuwa akamtafute aliyemuuzia
kiwanja hicho amrudishie fedha zake na kwamba umati ule umekuja
kuchukua eneo lao ambalo ni mali ya waislamu.
“Mheshimiwa hakimu umati ule ulichukua matofali yale na kuyapeleka eneo
la Markas na umati ule uliendelea kudumu katika kiwanja hicho toka
Oktoba 12 hadi 16 mwaka jana alfajiri ambapo polisi walikuja kuwakamata na
wakati wameweka kambi kwa siku hizo zote katika kiwanja hicho,umati huo
ulikuwa umefunga vipaza sauti katika eneo hilo ambapo wakulikuwa
wakitangaza eneo lile lilokuwa limetobolewa
kwaajili ya kujenga ukuta wa kutenganisha msikiti na markas lizibwe kwa
matofali yale yale waliyoyakuta pale na wakavunja na kibanda cha mabati”alidai Milanzi.
Kwa upande wake hakimu Nongwa aliairisha kesi hiyo hadi Februali
14 itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kusema kuwa siku hiyo aletwe
Ponda na mshtakiwa wa tano tu, Mkadamu ndiyo waletwe mahakamani
kwasababu wanaishi gerezani na kwamba washtakiwa waliosalia wasije
mahakamani kwasababu wanadhamana na akasema kesi hiyo itakuja tena
Februali 18,25,27 na 28 mwaka huu, kwaajili ya shahidi wa nane wa upande
wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wake, na kuamuru Ponda na Mkadamu
warudishwe gerezani kwasababu Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk.Eliezer
Feleshi bado hajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana washtakiwa hao.
Hata
hivyo jana hali ya usalama iliimalishwa kwa kiwango kikubwa
ukilinganisha na Januari 17 mwaka huu, kesi hiyo ilipokuja kwaajili ya
kusikilizwa, kwani zaidi wafuasi wa Ponda 200 walikuwa wamefurika ndani
ya viwanja vya mahakama hiyo na walijipanga katika viwanja hivyo
wakisubiri basi la Jeshi la Magereza lilokuwa limembeba Ponda na Mkadamu
lipite kwaajili ya kuwapeleka gereza la Segerea, ndipo umati huo
ulianza kupaza sauti ya juu kwa kusema ‘Takbir Allahwakbar,Takbir Allahwakbar’, huku wengine wakilisogelea basi alilokuwa amepanda Ponda.
“Nyie
Polisi mmezidi sana, sasa kwa taarifa yenu kesho (leo) mjiandae kutuua
sana kwa risasi, tunasema mjiandae kutuua kwa risasi…..serikali ya awamu
ya nne ina wapendelea sana wakristo na inatugandamiza waslamu,
tumechoka “walisikika wafuasi hao waliokuwa wamevalia kanzu na
baraghashia wakisema.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Februali Mosi mwaka 2013.
4 comments:
Heгe is my homeρage :: payday loan online
My website :: payday loan online
Нere is my hοmеpage payday loan,
Feel free to surf my web site ... payday loan online
Nice blog here! Also your site loads up fast! What web host
are you using? Can I get your affiliate link to your host?
I wish my site loaded up as fast as yours lol
Also visit my site How to get rid of static cling
My web page How to get rid of static electricity
I am in fact delighted to read this blog posts which carries plenty of valuable
information, thanks for providing these kinds of data.
Here is my web site ... Biotin for Hair Growth Reviews
Also see my page :: Biotin for Hair Growth Reviews
Post a Comment