SHEIKH MUKADAM AUNGANISHWA KESI YA PONDA
Na Happiness
Katabazi
KIONGOZI wa Jumuiya
na Taasisi za Kiislamu nchini,Mukadam Abdal Swalehe (45), jana alijikuta
akifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es
Salaam,akiunganishwa katika kesi ya
jinai Na.245/2012 inayomkabili Katibu wa Jumuiya hiyo ,Sheikh Issa Ponda Issa
na wenzake 49 wanaokabiliwa na makosa ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye
thamani ya Sh. milioni 59 na hivyo kufanya sasa kesi hiyo kufikia idadi ya
washtakiwa 51.
Sambamba na hiyo
Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Elezer Feleshi aliwasilisha mahakamani hapo
hati ya kumfungua dhamana Mukadamu kwaajili ya maslahi ya taifa chini ya
kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002.
Mukadam alifikishwa
jana mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa ambaye ndiye anayeisikiliza kesi
hiyo tangu mwanzo ambapo wakili
Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka
aliianza kwa kuieleza mahakama hiyo kuwa upande wa jamhuri unaomba
kuifanyia marekebisho hati ya mashitaka ya kesi ya jinai Na. 245/2012 kwasababu
imemuongeza mshitakiwa mmoja ambaye ni Mukadam na kwamba Mukadamu anakabiliwa na makosa
manne.
Wakili Kweka alidai
kuwa kosa la kwanza ni la kuingia kwa nguvu kwenye kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda
kosa kinyume na kifungu cha 85 na 35 cha
Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Oktoba 12 mwaka huu huko
Chang’ombe Markas, wasipokuwa na sababu za msingi waliingia kwa jinai kwenye
kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza Ltd, kujimilikisha kiwanja
hicho kwa njia ya iloyopelekea uvunjifu wa amani,wizi ambapo baada ya kufamia
waliiba vifaa na malighafi ikiwemo nondo, kokoto zenye jumla ya thamani ya Sh.
59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza na kosa la tano ni la uchochezi kinyume
na kifungu cha 390 na 35 cah sheria ya Kanuni ya Adhabu, ambalo sasa kosa hili
la uchochezi litamkabili Mukadamu na Ponda peke yao kuwa akiwa ni kiongozi wa jumuiya hiyo ,
Oktoba 12 mwaka huu ,aliwashawishi katika eneo hilo ambapo aliwaamasisha
washitakiwa hao watende kosa hilo.
Mshitakiwa huyo
alikana mashitaka yote,Wakili Kweka alisema DPP.Feleshi amewasilisha hati ya
kufunga dhamana ya Mukadamu na kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika tangu
Novemba Mosi mwaka huu na kwamba Novemba 15 mwaka huu, kesi Mukadamu na wenzie
50 watakuja kusomewa maelezo ya awali.
Kwa upande wake
hakimu Nongwa alisema makosa yanayomkabili mshtakiwa huyo yana dhamana ila
kwakuw DPP-Feleshi amewasilisha hati ya kumfungia dhamana, mahakama imefungwa
mikono,haiwezi kutoa dhamana kwasababu sheria iliyotumiwa na DPP kumfungia
dhamana mshtakiwa huyo na Ponda zimetungwa na Bunge, mahakama yenye ipo
kwaajili ya kuzifuata sheria hizo zilizotungwa na bunge katika kutoa uamuzi
hivyo akaamuru mshitakiwa huyo amepelekwe gerezani hadi hadi Novemba 15 mwaka
huu, kesi hiyo itakapokuja kwaajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Jana washitakiwa 49
katika kesi hiyo waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana
isipokuwa Ponda peke yake ambaye naye dhamana yake imezuiwa na DPP ambapo hivi
sasa ni washtakiwa wawili kati
ya 49 ndiyo dhamana zao zimefungwa na DPP, yaani Ponda na Mukadam ambao
watakuwa wakiendelea kusota gerezani.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 9 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment