VIONGOZI MTAA WA KIBASILA KORTINI KWA UHUJUMU UCHUMI
Na
Happiness Katabazi
VIONGOZI
wawili wa serikali ya mtaa wa Kibasila jijini Dar es Salaam na Mfanyakazi wa Benki
ya NMB, tawi la Kibasila wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 41, likiwemo la
uhujumu uchumi na wizi wa Sh.Milioni 18.6 mali ya serikali ya mtaa wa
Kibasila.
Mbali
na mashtaka hayo, pia wanakabiliwa na mashtaka ya kughushi, matumizi
mabaya ya nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri wao na wizi wakati wakiwa watumishi wa Umma.
Waendesha
Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Salha
Abdallah na Sophia Gulla mbele ya Hakimu
Bingi Mashabala waliwataja washitakiwa hao kuwa ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa
Kibasila, Aboubaker Maddy, Katibu wake, Stephen Mtangi na mfanyakati wa benki
ya NMB tawi la Muhimbili, Dorca Mtaita na kudai kuwa washtakiwa hao walitenda
makosa hayo kati ya Mei 13, mwaka 2006 na Desemba 10, mwaka 2008.
Wakili
huyo alidai kuwa mshtakiwa Maddy na
Mtangi wakiwa ni waajiriwa wa serikali
ya Mtaa wa Kibasila na kwamba walitumia
dhamana ya serikali waliyopewa kudanganya wakubwa wao kwa kutumia hati ya benki ya Desemba 10,
2008 kuonyesha maelezo ya uongo ya akaunti namba SA 2092502906 ya NMB
tawi la Muhimbili.
Aidha
mawakili hao wa Takukuru walidai kuwa pia washtakiwa hao walitenda kosa
kuisababishia serikali ya Mtaa wa Kibasila ya Sh 18,640,200 kutokana na
kughushi nyaraka kinyume na kifungu cha 333, 335 na 337 vya
Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Kuhusu
mfanyakazi wa NMB, Abdallah alidai kuwa Desemba 10, mwaka 2008 ,
Dorca akiwa mwajiriwa katika benki ya NMB tawi la Muhimbili
alighushi hati ya benki hiyo na kuonyesha kuwa akaunti ya
serikali ya mtaa wa Kibasila yenye namba SA 2092502906 ina Sh 18,009,379.13
wakati akijua kuwa ni uongo na kwamba akufanya hivyo alimsadia Maddy
kutenda kosa.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, washtakiwa wote walikana na upande wa mashtaka
ulidai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Na
kwa upande wake Hakimu Mashabala alisema ili kila mshtakiwa apate dhamana ni
lazima awe na wadhamini wawili wenye
vitambulisho na barua ambapo kila mdhamini
alitasaini bondi ya Sh.milioni tatu.Washitakiwa
hao waliweza kutimiza masharti hayo na hakimu Mashabala aliwapatia dhamana na
akaairisha kesi hiyo hadi Januari 5, mwaka huu itakapokuja kwaajili ya
kutajwa .
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 22 mwaka 2012.
|
2 comments:
Аctually no matter if someοne ԁoesn't know after that its up to other visitors that they will assist, so here it occurs.
My web page Same Day Payday Loans
Ηaving гeаԁ this I thought іt was rather
еnlightenіng. I аρpreciаtе you finding the time anԁ effοrt tо put thіs
іnfoгmatіve аrtіcle together.
I oncе agаin find myself personally spending way too muсh timе both reading аnd commenting.
But ѕo what, it was ѕtill ωorthwhіlе!
Fеel freе tο suгf to my web
blog: New Bingo Sites
Post a Comment