ATIWA HATIANI KWA MAKOSA YA KUFANYA BIASHARA HARAMU YA KUSAFIRISHA BINADAMU
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imemtia hatiani mfanyabiashara wa ngozi
nchini, Salim Ally (61) kwa makosa ya kusafirisha binadamu na kuwatumisha na
kumhukumu kwenda jela miaka 10 au kulipa fidia ya jumla ya milioni 17.
Hukumu hiyo
ya kesi hiyo ya ki historia na ya kwanza kutolewa katika Mahakama hiyo tangu
Sheria ya Usafirishaji haramu binadamu ya mwaka 2008 ilipotungwa na bunge,
ilitolewa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ilvin Mugeta.
Akitoa
hukumu hiyo hakimu Mugeta alisema upande
wa jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali Arafa
Msafiri, Prosper Mwangamila na Hamid Mwanga katika kujenga kesi yao walileta
jumla ya mashahidi watano wakati mshtakiwa aliyekuwa akitetewa na wakili wa
kujitegemea Majura Magafu alijitetea yeye mwenyewe bila kuleta shahidi yoyote.
Hakimu
Mugeta alianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa ilidaiwa mahakamni hapo na
upande wa jamhuri kuwa Agosti 8 mwaka 2010 alimsafirisha Abduswamad na wenzake
kwenda nchini Yemen na kwenda kuwatumisha kwa nguvu na bila ya kuwalipa ujira
wao kinyume na kifungu cha 4(1)a,6(2)c, cha Sheria ya Usafirishaji haramu wa
binadamu ya mwaka 2008.
Alisema
baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili na vielelezo ,mahakama yake
imefikia uamuzi wa kuona upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kesi yake na
kwamba baadhi ya ushahidi uliotolewa na mshtikakiwa na wakili wa Magafu ulikuwa
unatofautiana kwani Magafu katika majumuisho yake alidai Abduswamad alijisafirisha mwenyewe kwenda Yemen
akusafirishwa na mshtakiwa lakini Mshtakiwa katika utetezi wake alidai yeye
aliwasaidia fedha washtakiwa kwenda Yemen kwasababu washtakiwa hao walikuwa
wakiitaji fedha za kwenda Yemen kufanyakazi kwa mtu mwingine na yeye akaamua
kuwapatia kwa makubaliano kuwa wakimaliza kufanyakazi kwa mtu huyo wataenda
kufanyakazi kwenye nyumba yake iliyopo Yemen na kwamba fedha hizo alizowaazima
watakuwa wakimlipwa katika fedha watakazokuwa wanalipwa kutoka kwa mtu
waliyokuwa wamekwenda kumjengea nyumba.
“Mahakama
hii inasema upande wa jamhuri umeweza kuthibitisha kesi yake kwani ushahidi
ulitolewa ambao upande wa utetezi umeshindwa kuupinga umetosha kuifanya
mahakama hii iamini kuwa ni mshtakiwa ndiye aliyewasafirisha watu hao kutoka
Tanzania kwenda Yemen kuwatumisha bila kuwa ujira na kwasababu hiyo mahakama
hii inamtia hatiani kwa makosa hayo”alisema hakimu Mugeta.
Baada ya
kumtia hatiani wakili Msafiri alidai mahakama haina rekodi ya mshtakiwa ambayo
inaonyesha ni mhalifu mzoefu na kwasababu hiyo hii ni kesi yake ya kwanza
kutiwa hatiani na kwamba anaomba mahakama imwamuru mshtakiwa amlipe faini waathirika(waliosafirishwa) na itoe
adhabu stahili.
Kwa upande
wake wakili mshtakiwa, Magafu aliomba mahakama isimpe adhabu ya kwenda
kutumikia kifungo gerezani kwani mshtakiwa ni mtu mzima sana,ana matatizo ya
kiafya na kwamba akifungwa jela ,watanzania watapata hasara kwasababu kodi zao
zitatumika kumtunza wakati mshtakiwa huyo hawezi kufanya kazi ngumu.
Aidha Hakimu
Mugeta alisema amesikiliza maombi ya mawakili hao na kwamba ana mwamuru Ally
kwenda jela miaka 10 au kulipa faini ya Sh.milioni saba pamoja kumlipa fidia
Abduswamad na mwenzake sh milioni 10.
Hata hivyo ndugu wa mshtakiwa walilipa kiasi hicho cha fedha na hivyo kumfanya mshtakiwa huyo aliyesota gerezani kwa zaidi ya miezi nane sasa kuwa huru.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 29 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment