KG.210 ZA PEMBE ZA NDOVU ZAWAFIKISHA KIZIMBANI
Na Happiness Katabazi
WATU wanne
jana walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,
wakikabiliwa na makosa mawili ya kumiliki Kg.210 za Pembe za Ndovu bila kibali
na kusaidia washitakiwa kutenda kosa.
Wakili wa
serikali Hamidu Mwanga mbele ya Hakimu Mkazi Stewart Sanga aliwataja
washitakiwa hao kuwa Peter Kabi,Leonida Loi Kabi, Charles Wainaina na Polisi
Malisa.
Wakili
Mwanga alidai shitaka la kwanza kwaajili ya washitakiwa wote ni la kukutwa wakimiliki nyara za serikali
kinyume na kifubgu cha 86(1), 2(2) na 3 cha Sheria Uhifadhi wa Wanyapori Na.5 ya mwaka 2009 kinachosomwa pamoja na kifungu cha 57(1) na mstari wa 14(d) katika jedwali la kwanza pamoja na
sheria Economic And Organazation Crime Control Act ya mwaka 2002.
Kuwa Novemba
11 mwaka huu, huko eneo la Kimara Dar es Salaam walikutwa wakimiliki pembe za Ndovu zenye uzito wa Kg.210 zenye thamani ya dola
za Kimarekani 247,830,000 ambazo wakati huo
zilikuwa na thamani ya Sh
391,571,400 na vipande vitano vya mifupa ya Tembo zenye thamani ya dola za
Kimarekani 30,,000,000 wakati huo zilikuwa na thamani ya sawa na Sh
47,400,971,400 mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila leseni.
Wakili
Mwanga alidai shitaka la pili ni kwaajili ya mshtakiwa wa tatu na wanne(Charles
Wainaina na Polisi Malisa) , ambalo ni la kuwasaidia washitakiwa kutenda kosa
kinyume na kifungu cha 387 cha Sheria ya
Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, ambapo alidai kuwa Wainaina na Malisa kuwa Oktoba
27 mwaka huu, huko katika Kituo cha
Polisi Kimara huku wakijua kuwa
mshitakiwa wa pili(Leonida Loi Kabi)
alikuwa amekamatwa kwa tuhuma za kukukutwa akimiliki mali nyara za serikali , alimsaidia Kabi kwa
kuwashawishi polisi kwa lengo la kumuweza Kabi atoroke ili
asiadhibiwe, na kwamba upelelezi bado haujakamilika.
Hata hivyo
washtakiwa wote walikanusha mashtaka hayo na hakimu Sanga alisema jana hawezi
kutoa masharti ya dhamana na akaamuru washitakiwa wapelekwe rumande hadi Novemba
12 mwaka huu, ambapo siku hiyo ndiyo atatoa masharti ya dhamana.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Agosti 9 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment