MAOFISA WA TAZARA KIZIMBANI
Na Happiness
Katabazi
MAOFISA
wawili wa TAZARA jana walifikishwa
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na makosa
mawikili likiwemo la kusababishia TAzara sh milioni 120.
Mbele ya
Hakimu Mkazi Frank Moshi wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka aliwataja
washtakiwa hao kuwa ni Mhandisi Mkuu wa Mitambo , Wenceslaus Kamugisha na Meneja Mkuu wa Fedha wa Tazara, Sarah
Masiliso.
Wakili Kweka
alidai shtaka la kwanza ni la matumuzi mabaya ya madaraka ambalo ni kinyume na
kifungu cha 31 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007, kuwa
mnamo Aprili mwaka 2011, wakiwa ni
waajiliwa wa kwa nyadhifa hizo kwa
makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kupitisha maombi katika mchakato wa
tenda kinyume na sheria na kwa malengo
ya kuipatia faida kampuni ya Chrinkap Indutrial.
Wakili Kweka
alidai kosa la pili ni la kusababisha hasara
ambalo ni kinyume na mstari wa 10(1) ya jedwari la kwanza na kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu uchumi.
Kwamba
Aprili mwaka 2011 katika maeneo ya Ilala
jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa
ni waajiliwa wa Tanzania, Zambia Lairway Authority kwa makusudi waliisababishia serikali ya
Tanzania hasara y ash 120,000,000.
Hata hivyo
washtakiwa hao walikana mashtaka na
hakimu Mosha alisema ili wapate dhamana ni lazima kila mshtakiwa awe na wadhamini wa wili ambao wanafanyakazi
katika taasisi zinazotambulika na serikali na kwamba wadhamini mmoja atasaini bondi ya Sh.milioni 10 na kwamba
mdhamini mmoja au mshtakiwa ataweka
mahakamani fedha taslimu sh milioni 30
au hati ya mali isiyoamishika yenye thamani hiyo ya milioni 30.
Lakini hata
hivyo mdhamini mmoja aliwasilisha hati ya mali isiyoamishika yenye thamani y
ash.milioni 62 ambayo aliomba hati hiyo itumike kuwadhamani washtakiwa wote
ombi ambalo lilikubuwaliwa na hakimu hiyo licha wakili Kweka aliomba mahakama
iupatie muda upande wa jamhuri uende kuikagua hati hiyo ,na hakimu alikubali
hoja hiyo akaiarisha kesi hiyo hadi leo ilikuja kuona kama washtakiwa walikuwa
wametimiza masharti hayo ya dhamana.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 27 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment