RUFAA YA GODBLES LEMA KUANZA DESEMBA 4
Na
Happiness Katabazi
MAHAKAMA
ya Rufani nchini , Desemba 4 mwaka huu, itaanza rasmi kusikiliza rufaa iliyokatwa na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo
la Arusha Mjini(Chadema), Godbless Lema,
ya kupinga hukumu ya MAhakama Kuu Kanda ya Arusha ambayo ilimvua ubunge Lema.
Kwa
mujibu wa ratiba ya vikao vya mahakama ya Rufani, inaonyesha uongozi wa
mahakama hiyo upanga jopo la majaji watatu watakao sikiliza kesi hiyo ambao ni
Jaji Salum Massati, Natharia Kimaro na Bernad Luanda ambao kikao kitaketi
jijini Dar es Salaam, kuanzia saa tatu asubuhi.
Kupwangwa
kwa rufaa hiyo kuanza kusikilizwa tarehe hiyo kumekuja baada ya Lema
kuwasilisha rufaa yake upya ambayo ameifanyia marekebisho kama alivyoamliwa na
mahakama hiyo Novemba 8 mwaka huu,
ambapo mahakama hii ilikataa ombi la wajibu maombi katika rufaa hiyo waliyotaka
Mahakama hiyo iifute rufaa ya Lema kwa sababu ina mapungufu badala yake
mahakama hiyo ilikiri kuaini mapungufu katika rufaa ya Lema lakini ikasema
mapungufu hayo hayawezi kuifanya mahakama ifikie uamuzi wa kuifuta rufaa ya
Lema kwani mapungufu hayo yalifanywa na watendaji wa mahakama ambao ndiyo
waliandaa rufaa hiyo na ikampatia Lema siku 14 kuanzia siku hiyo awe
amewasilisha upya rufaa yake aliyoifanyia marekebisho.
Aprili
5 mwaka huu, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilitoa hukumu yake na kumvua ubunge
Lema
Lema
kufuatia kesi iliyofunguliwa na
wanachama watatu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo
na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu mwaka 2010.
Lakini
baadaye, alikata rufaa Mahakama ya Rufani, kupitia kwa wakili wake Method
Kimomogoro kupinga hukumu ya Mahakama Kuu, huku akitoa hoja 18 za kupinga
hukumu hiyo.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Novemba 27 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment