KESI YA SHEIKH PONDA KUANZA KUSIKILIZWA NOVEMBA 29
Na Happiness Katabazi
KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh
Ponda Issa Ponda na wenzake 49,jana walikanusha
madai ya upande wa jamhuri katika kesi ya uchochezi na wizi wa Sh
milioni 59 katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kuwa Baraza Kuu la Waislamu nchini(BAKWATA), siyo
chombo cha kuwakilisha waislamu wote hapa nchini.
Wakili wa washitakiwa hao
Mansoor Nassor mbele ya Hakimu Mkazi Victoria Nongwa ndiye alikanusha madai
hayo kwa niaba ya washitakiwa muda mfupi baada ya Wakili Mwandamizi wa Serikali
Tumaini Kweka kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao ambapo ndani ya
maelezo hayo alidai BAKWATA ni chombo kinachotambuliwa na serikali na kipo
kwaajili ya kuwawakilisha waislamu wote.
“Mheshimiwa hakimu wateja
wangu wamenituma nikanushe madai ya kuwa BAKWATA ni chombo kinachotambulika na
serikali na kipo kwaajili ya kuwawakilisha waislamu wote”alidai wakili Mansoor.
Kama ilivyo ada ya kesi
hiyo ijapo mahakamani hapo, ulinzi mkali ulitawala tangu saa 12 asubuhi
ndani,na nje ya viwanja vya mahakama hivyo ambapo wanausalama walisimama getini
wakiwa na vifaa maalumu vinavyoweza kumtambua mtu ambaye amebeba silaha
zinazoweza kuhatarisha usalama pia ndugu na wadhamini wa washitakiwa hao huku
wakiwa wamevalia mavazi ya kanzu na Baibu walianza kumiminika tangu saa 12:30
asubuhi ndani ya viwanja vya mahakama hiyo na kesi hiyo ikaanza kusikilizwa saa
9:011 asubuhi ambapo Ponda na Mkadamu waliletwa asubuhi na maofisa wa jeshi la
Magereza waliokuwa wamevalia mavazi maalum ya kujikinga na hatari yoyote, gari
la maji ya kuwasha “Kikojozi” gari za
polisi aina ya defenda nne zilizokuwa zimejaa askari wa kikosi cha kutuliza
ghasia zilimleta na kurudisha gerezani Ponda na Mukadamu.
Kabla ya kuwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao,
wakili Kweka alianza kwa kuimbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja
kwaajili ya kubadilisha hati ya mashtaka kwasababu wanamuongeza mshtakiwa mmoja
ambaye ni Kiongozi wa taasisi inayoongozwa Ponda, Mukadam Abdal Swalehe(45)
ambaye amekuwa mshtakiwa wa tano katika kesi hiyo ya jinai Na.245/2012 na pia
Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi amewasilisha hati ya kumuondoa mshitakiwa
35 katika kesi hii Rashid Omary chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Makosa
ya Jinai ya mwaka 2012, kwasababu hana haja ya kuendelea kumshtaki Omary hicho kufanya sasa hati ya mpya ya
mashtaka kuwa na washitakiwa 50 tu.
Baada ya kumaliza kutoa
maelezo hayo Wakili Kweka alianza kwa kuwasomea upya mashtaka yanayowakabili
ambapo alisema wanakabiliwa na makosa matano.
Kosa
la kwanza alidai ni la kula njama ambalo linawakabili washitakiwa wote,kosa la
pili ni kwaajili ya washitakiwa wote ambalo ni la kuingia kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume na kifungu
cha 85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, kuwa Oktoba 12
mwaka huu huko Chang’ombe Markas, wasipokuwa na sababu za msingi waliingia kwa
jinai kwenye kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza Ltd, kujimilikisha
kiwanja hicho kwa njia ya iloyopelekea uvunjifu wa amani,wizi ambapo baada ya
kuvamia waliiba vifaa na malighafi ikiwemo nondo, kokoto zenye jumla ya thamani
ya Sh. 59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza na kosa la tano ni la uchochezi
kinyume na kifungu cha 390 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, ambalo sasa
kosa hili la uchochezi litamkabili Mukadamu na Ponda peke yao kuwa wakiwa
ni viongozi wa jumuiya hiyo , Oktoba 12 mwaka huu ,waliwashawishi wafuasi wao
watende makosa hayo hata hivyo walikanusha mashtaka yote.
Akiwasomea maelezo ya awali
wakili Kweka alidai washtakiwa na makosa hayo na na kwamba BAKWATA ni taasisi iliyoundwa ili kutoa miongozo pamoja inatambulika kama inawawakilisha waislamu wote Tanzania.
Kwamba Baraza chini ya wadhamini wake ,BAKWATA inamiliki
mali kama viwanja na majengo
mbalimbali na miongoni mwa mali za
BAKWATA ni kiwanja kilichopo eneo la
Chang’ombe Markas Kitalu Na.311/3/4/Block T.
Wakili Kweka alidai Juni 18 mwaka 2011 ,BAKWATA kupitia wadhamini wake waliingia katika makubaliano ya
kupangisha kiwanja hicho cha Chang’ombe
kwa kampuni ya Agritanza Ltd kwaajili ya
kuuza au kubadilisha mali hiyo ambayo ni
kiwanja kwa kampuni hiyo.
“Mabadilishano hayo yaliyofanywa kati ya BAKWATA na kampuni ya
Agritanza yaliambatana na fedha na kubadilishana kiwanja kilichopo Kisarawe
mkoani Pwani na kutokaa na makubaliano hayo
ardhi ya kiwanja kilichopo Chang’ombe Markas kiliingizwa kisheria kwenye umiliki mpya wa
kampuni ya Agritanza’alidai Kweka
Ailiendelea kueleza kuwa Oktoba
12 mwaka huu, baada ya kampuni ya Agritanzaa kuanza kumiliki kiwanja hicho toka
mikononi mwa BAKWATA , kampuni hiyo ilianza kukiendeleza kiwanja hicho ambapo wafuasi wa wa Baraza Kuu la Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu, katika hali ya uvunjifu wa amani walivamia kiwanja hicho
wakiongozwa na Ponda na mshitakiwa wa tano(Mukadamu).
Wakili Kweka alidai baada ya
washtakiwa hao kuvamia kiwanja hicho
walikaa kwenye kiwanja hicho kuanzia Oktoba 12-16 mwaka huu hado Oktoba
16 mwaka huu na wakaaribu msingi uliokuwa umeanza kujengwa na kampuni hiyo na malighafi zilizokuwa zimeifadhiwa kwenye
kiwanja hicho kwaajili ya ujenzi na katika uhalifu huo washitakiwa hao walikuwa
wakiongozwa na Ponda na Mukadamu na kwamba tukio lilipotiwa polisi Oktoba 16
na washtakiwa walikamatwa na polisi wakiwa katika eneo hilo ambapo Oktoba 18 mwaka huu, walifunguliwa
kesi mahakamani hapo.
Akipangua maelezo hayo ya
awali, wakili wa washitakiwa Mansoor alianza kwa kudai kuwa wateja wake
wanakanusha maelezo kuwa BAKWATA ni taasisi inayotambuliwa na serikali na ipo
kwaajili ya kuwawakilishwa waislamu wote na pia wanakanusha kuwa Mukadamu hakufikishwa
mahakamani hapo Oktoba 18 mwaka huu, Mukadamu alifikishwa mahakamani hapo kwa
mara ya kwanza Novemba 8 mwaka huu na kwamba anaomuombe Mukadamu dhamana
kwasababu makosa anayokabiliwa nayo leo yana dhamana.
Wakili Mansoor pia aliomba
upande wa jamhuri uzingatie haki za msingi za Ponda kwani wanazifunja haki za
kiongozi huyo wa kiroho ambapo wanamfunga pingu hadi anapomuingiza ndani ya
chumba cha mahakama na kwamba wanaomba upande wa jamhuri uwapatie maelezo ya
mlalamikaji na orodha ya majina ya mashahidi watakaowaleta kutoa ushahidi.
Akipangua hoja hizo kwa
vielelezo wakili wa serikali Kweka alieleza kuwa kuhusu ombi la kuwapatia
upande wa utetezi majina ya mashahidi na vielezo tutakavyotumia katika kesi
hizo haliwezekani kwasababu tayari kuna maamuzi mbalimbali yaliyokwisha tolewa
na Mahakama ya Rufaa nchi ambayo yameeleza wazi kuwa upande wa jamhuri
haulazimiki kuwapatia upande wa utetezi majina ya mashahidi wake na vielelezo
vyake na kuongeza kuwa kifungu cha 192 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka
2002 , haielezi kuwa upande wa jamhuri unapomaliza kuwasomea maelezo ya awali
washitakiwa ni lazima uwapatie majina washitakiwa majina ya mashahidi na
vielelezo.
Aidha kuhusu hoja iliyoomba
Mukadamu apatiwedhamana leo ,wakili Kweka alidai Mukadamu alifunguliwa kesi
Novemba 8 mwaka huu na siku hiyo DPP aliwasilisha hati ya kufunga dhamana yake
chini ya kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Makosa ya Jinai, na kwamba DPP bado
hajaiondoa hati hiyo na kwamba jamhuri ni sikivu sana na kwamba wameipokea hoja
ya wakili Mansoor kuhusu kutotaka Ponda afungwe pingu mikononi hadi akiwa
anaingizwa ndani ya chumba cha mahakama.
Kwa upande wake Hakimu Nongwa
alieleza kuwa DPP bado hajaondoa hati ya kufunga dhamana ya Mukadamu aliyoiwasilisha
Novemba 8 mwaka huu,na kwamba hati hiyo bado ipo kwenye kumbukumbu za mahakama na ndiyo masharti ya dhamana hayajabadilika na
kwamba hivi sasa Ponda na Mukadamu katika kesi hiyo ndiyo wataendelea kusota
rumande kwasababu DPP bado ameendelea kufunga dhamana yake na kuongeza kuwa
maofisa usalama watumie njia nyingine za kumlinda Ponda siyo kumfunga Pingu
mkono Ponda hadi wanapomuingiza ndani ya chumba cha mahakama.
Aidha hakimu Nongwa aliushauri
upande wa Jamhuri ulete idadi ya jumla ya mashahidi wanaokusudia kuwaleta kutoa ushahidi katika
kesi hiyo na kuarisha shauri hilo hadi Novemba 29 mwaka huu, itakapokuja
kwaajili shahidi wa kwanza wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wake.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 16 mwaka
2012.
No comments:
Post a Comment