Header Ads

RUFAA YA DPP V ZOMBE KUSIKILIZWA DECEMBA 11


Na Happiness Katabazi

MAHAKAMA ya Rufani nchini imepanga kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam , ilimwachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam,Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe na wenzake  itaanza kusikilizwa Desemba 11 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ratiba ya vikao iliyotolewa na mahakama hiyo inaonyesha rufaa hiyo inayosubiriwa kwa shauku kubwa na umma itaanza kusikilizwa kuanzia saa tatu asubuhi mahakamani hapo jijini Dar es Salaam.

Aidha ratiba hiyo ya vikao inaonyesha jopo la majaji watatu ambao ni Jaji William Mandia, Nathalia Kimaro na Jaji Katherine Oriyo ndiyo wamepangwa kuikisiliza rufaa hiyo Na. 254/2009 iliyokatwa na DPP ,Dk.Feleshi   Oktoba 6, 2009.

Ambapo katika rufaa hiyo DPP ametoa sababu 11 za kukata rufaa ambapo alidai Jaji Massati alikosea kisheria kuwaachiria huru washtakiwa  na kwamba anaiomba mahakama ya rufaa itengue hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na Jaji Massati  Agosti 17 mwaka 2009 , kwasababu ina mapungufu mengi ya kisheria na jaji huyo alijielekeza vibaya katika kutoa hukumu ile iliyowaachilia huru washtakiwa.

Walikuwa wakidaiwa kuwa kutenda makosa hayo tahere 14 Januari 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Jijini Dar es Salaam.

Wafanyabiashara hao ni Sabinus Chigumbi, au Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe pamoja na Juma Ndugu, dereva teksi.

Mbali na Zombe aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea Jerome Msemwa, washtakiwa wengine walikuwa ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Noel Leonard, Konstebo Jane Andrew, Koplo Nyangerela Moris, Konstebo Emanuel Mabula na Koplo Felix Sedrick,

Wengine walikuwa ni Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rashid Lema (aliyefariki kabla ya kujitetea), Koplo Rajabu Bakari na Koplo FestusGwabisabi.
  
 Chanzo;Gazeti la Tanzania Daima la Jumatatu, Novemba 19 mwaka 2012.

2 comments:

Anonymous said...

I think this is one of the mοst importаnt infο foг mе.

And i аm glаd reading your artiсle.
But wannа remarκ on few general things, The ωeb site style is ideаl,
the aгticles is really excеllent : D. Good ϳоb,
cheerѕhttp://sоundclouԁ.cοm/usеr58513297/watch-criminal-mindѕ-season-8
my web site > Criminal Minds Season 8 Episode 8

Anonymous said...

I abѕolutely loѵe your site.. Pleasаnt colorѕ & themе.
Did you devеlop thiѕ ѕite уouгself?
Pleaѕe геply baсk as
I'm looking to create my very own blog and would love to know where you got this from or exactly what the theme is named. Kudos!Private Practice Season 6 Episode 7 The World According to Jake
my webpage: Private Practice Season 6 Episode 7 The World According to Jake

Powered by Blogger.