PRO.KAPUYA KULISHTAKI DIRA KWA KUMSINGIZIA KAFICHA FEDHA ZA SERIKALI NJE YA NCHI
Na Happiness Katabazi
WAZIRI wa Mstaafu wa Wizara ya Ulinzi ,Profesa Juma Kapuya amelitaka Gazeti la Dira limlipe fidia ya
bilioni tano na limuombe radhi ndani ya
siku 14 kuanzia sasa ama sivyo atalifikisha mahakamani gazeti hilo kwa
kuchapisha habari ya uongo dhidi yake kuwa ameiba fedha za umma na kwenda
kuzificha katika benki ya Switzeland
kwasababu habari hiyo imemletea madhara na kumshushia heshima yake.
Profesa Kapuya
kupitia wakili wake Yassin Memba tayari ameishalikabidhi gazeti la Dira
kusudio hilo ambapo nakala ya kusudio hilo ambalo gazeti hili linayonakala yake
Kapuya anasema gazeti hilo linalochapishwa mara moja kwa wiki katika
toleo lake Na.207 la Jumatatu ya Novemba
12-18 ya mwaka huu, lilichapisha habari ya kumkashfu na ndiyo maana analitaka
gazeti hilo limuombe radhi ndani ya siku 14 kaunzia sasa.
Wakili Memba alisema habari hiyo iliyomkashfu mteja wake ni
ile iliyochapishwa ukurasa wa mbele ambayo ilikuwa na kichwa cha habari
kisemacho; “VIGOGO WA MABILIONI YA USWISS HAWA HAPA”.
Alisema kichwa hicho cha habari ambacho kilikuwa kimepambwa
na picha ya vigogo hao ikiwemo Picha ya mteja wake (Profesa Kapuya) ambayo ni
kama ushahidi wa habari hiyo ambayo ilipandishwa ukurasa wa kwanza, na mstari
wa 16,17 na 18 ambazo zilikuwa zikisomeka kama ifuatavyo:
“Zitto alieleza zaidi
kuwa wengine ambao mali zao zinapaswa
kuchunguzwa kwa kina na Serikali ni waliopata kushika wadhifa
wa uwaziri wa ulinzi na ukuu wa majeshi katika kipindi hicho
cha mwaka 2003 hadi 2010.
“Mawaziri waliopata
kuiongoza Wizara ya Ulinzi katika kipindi hicho ni
pamoja na Profesa Philemoni Sarungi, Profesa Juma Kapuya na Edgar Maokola Majogo na wakuu wa
Majeshi walikuwa Jenerali Robert Mboma
na Jenerali Geogre Waitara. Majina ya
vigogo jawa waliopata kuongoza wizara ya ulinzi katika serikali ya Rais Mstaafu Benjamin
Mkapa yanaingia katika mlolongo wa
majina yanayotakiwa na Zitto kufanyiwa uchunguzi wa kina
wa mali zao na Serikali kutokana
na kuwa madarakani wakati
kampuni ya Meremeta ambayo baadaye ilibadilishwa jina kuitwa
TanGold iliyokuwa
ikifanyakazi chini ya Jeshi
kudaiwa kutorosha mabilioni ya fedha nje
ya nchi”.
Wakili Memba alisema mstari Na. 28 wa habari hiyo ulikuwa na
maneno yanayosomeka hivi; “Fedha
zilizoibwa na kutoroshwa kupitia
kampuni ya Meremeta na kampuni ya Deep
green ziliishia kwenye akaunti za
watu binafsi nje ya nchi.Hata hivyo mara baada
ya kuundwa kwa kampuni ya
TanGold, jumla ya dola za Kimarekani
milioni 10 ziliwekwa kwenye akaunti
ya kampuni hiyo katika Benki ya NBC, Tawi la Corporate
.Nambari ya akaunti hiyo poa itatolewa katika kamati ninayoomba
kuunda kwa ajili ya uchunguzi wa
kina”.
“Hayo maneno yaliyochapishwa kwenye hiyo habari kuhusu
Kapuya ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi wa zamani kuwa aliamisha fedha za
serikali kinyume cha sheria na kwenda kuzificha katika benki huko nchini
Switzerland, na habari hiyo ya uongo ilikuwa na lengo la kumchafulia jina mteja
wangu na kumshushia heshima yake na
kumchonganisha na wananchi na imemletea
madhara ya kiafya na kumsababishia usumbufu mkubwa na
tangia ilipochapishwa hiyo habari mteja wangu anataka gazeti lako limlipe
Sh.bilioni tano kama fidia ya madhara aliyoyapata tangu habari hiyo
ilivyochapishwa”alisema Wakili Memba.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Novemba 28 mwaka 2012.
No comments:
Post a Comment