Header Ads

SERIKALI YAMUANIKA IDD SIMBA MAHAKAMANI



Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kulisababishia Shirika la Usafiri Dar es Salaam(UDA), Mwenyekiti wa Bodi ya shirika hilo Idd Simba na wenzake umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam kuwa Simba  alitumia sehemu ya fedha za mauzo ya hisa zilizouzwa kwa Kampuni ya Simon Group  Limitedkununulia gari lake binafsi.

Mbali na Simba washtakiwa wengine ni Mkurugenzi wa Bodi ambaye aliwai kuwa Diwani wa Sinza na Katibu Mwenezi wa CCM,Mkoa wa Dar es Salaam, Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa Shirika hilo la Usafiri Victor Milanzi ambao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Ilvin Mugeta ,Mei 29 mwaka jana.

Wakili wa serikali Awamu Mbagwa alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya awali washtakiwa hao  ambapo aidai kuwa  Agosti 31, 2009, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Simon Group Limited, Robert Kisena aliwasilisha barua yake ya kusudio la kununua hisa 49 za serikali  kwa   uongozi wa UDA.
 Mbagwa alieleza kuwa  Septemba 2 mwaka  2009, mshtakiwa wa tatu(Milanzi) ambaye alikuwa ni Meneja Mkuu wa UDA alisaini barua ikiielekeza Simon Group, kuwasilisha malipo ya awali ya Sh milioni 400 kama ishara ya dhamira ya kununua hisa hizo.
“Pia barua hiyo ya Kisena  iliielekeza  kampuni ya Simon Group kuweka fedha  hizo katika akaunti binafsi namba 0210001002, inayomilikiwa na Simba katika benki ya Bank M, tawi la Sea View…..   na barua hiyo ilieleza zaidi  kuwa malipo hayo ya awali ya sh.milioni 400  yangejumuishwa katika ununuzi wa hisa hizo .”, alidai .

Alidai kuwa barua hiyo ilielekeza kuwa fedha hizo ziingizwe katika akaunti hiyo Simba ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa maelezo kuwa  akaunti za UDA zilikuwa na madeni mengi wakati mshtakiwa huyo akifahamu maelezo hayo ni ya uongo.


Wakili huyo alieleza kuwa kutokana na maelekezo hayo ya washtakiwa, Septemba 3, 2009, Kisena kwa niaba ya Simon Group aliingiza Sh milioni 250  katika akaunti namba 0210001002 iliyoko Benk M, Tawi la Sea View, inayomilikiwa na mshtakiwa wa kwanza (Idd Simba).

Wakili hiyo alidai kuwa fedha  hizo zilihamishwa kutoka katika akaunti namba 2046600338 inayomilikiwa na Robasika Agro Products iliyoko katika Benki ya NMB, kampuni ambayo Simon Group Limited ni mwanaisa wake na kwamba baada ya  baada ya fedha hizo  kuingizwa katika akaunti hiyo, siku hiyohiyo mshtakiwa wa kwanza, Simba, alitoa Sh milioni 100  kwa kutumia hundi namba 125293.

Alidai  na kwamba siku iliyofuata, Septemba 4, 2009,  Simba, alihamisha fedha hizo kutoka katika akaunti yake namba 0210001002, kiasi kingine cha Sh milioni 100  kwenda katika akaunti namba 0150000381 inayomilikiwa na kampuni ya Africarriers Ltd, katika Bank M.

“Kiasi hiki kilichohamishiwa kwa Africarriers kilikuwa ni sehemu ya malipo ya ununuzi wa gari aina ya Toyota Landcruser  VX lenye namba za usajili T 561 BCX, ambalo hivi sasa limesajiliwa kwa jina la mshtakiwa wa kwanza yaani Simba.”, alisisitiza Wakili Mbagwa.

Alidai kuwa awali kabla ya kuingizwa kabla kwa kiasi cha Sh cha Sh .milioni 250 , akaunti ya mshtakiwa ilikuwa na kiasi cha Sh 3,329,242.88 tu.

Kwa mujibu wa Wakili Mbagwa, Novemba 26, 2009, Kisena aliingiza kiasi cha Sh Milioni 30  katika akaunti namba 6033500127 inayomilikiwa na Pride Tanzania, Makambako, NMB, na baadaye Sh milioni 20  kwa maelekezo ya mshtakiwa wa kwanza.
 
Aliongeza kuwa  kiasi hicho cha fedha baadaye Desemba 4, 2009  na Januari 27, 2010, zilihamishiwa katika akaunti namba 4081300002, inayomilikiwa na Pride Tanzania, makao makuu ya NMB, mwisho wake  zinakaingizwa  katika akaunti binafsi ya mshtakiwa wa kwanza namba 0210001002 na mchakato huu wote ulifanyika kwa maelekezo ya Idd Simba..

Aliongeza kuwa baadaye Januari 22, 2010, Kisena aliingiza tena sh.milioni 20  katika akaunti namba 0210001002 ya mshtakiwa wa kwanza na hivyo kufanya jumla ya kiasi cha fedha zilizoingizwa na Kisena kwa niaba ya kampuni ya Simon Group Limited, katika akaunti binafsi ya mshtakiwa kama malipo ya utangulizi ya ununuzi wa hisa za UDA  ni Sh milioni 320….na hata hivyo  fedha hizi zote hazikufikishwa kwenye  akaunti za UDA badala yake ziliishia kutumiwa vibaya na mshtakiwa wa kwanza na wa tatu Simba na Milanzi.”

Alidai kuwa baada ya hayo yote kuwa yameshafanyika, Januari 28, 2010 katika mkutano wa Bodi ulifanywa na mshtakiwa wa kwanza, Simba na wa pili, Mwaking’inda, kwa makusudi na wakijua, walipitisha uamuzi wa kuuza hisa 7,880,303 za UDA kwa Simon Group, ambazo hazikutolewa kwa mauzo.

Alidai kuwa uamuzi huo wa Bodi ulofikiwa bila kufuata utaratibu wa zabuni yenye ushindani.

Wakili Mbagwa alidai kuwa kutokana na uamuzi huo, Februari 11, 2010, mshtakiwa wa kwanza na wa tatu kwa kutumia vibaya nafasi zao, walisaini mkataba wa makubaliano ya mauzo na Simon Group,  ya hisa 7,880,303 ambazo hazikuwa katika mchakato wa kuuzwa.

Alidai kuwa hisa hizo ziliuzwa kwa bei ya Sh.1,142,643,935,tu kwa bei ya Sh145 kwa kila hisa ambayo alidai kuwa ilikuwa ni chini ya bei ya soko  kwa wakati huo ambapo bei ilikuwa Sh 1513 kwa kila hisa na matokeo  washtakiwa waliisababishia UDA hasara Sh 8,422,076,940 (Sh8.4 bilioni).”, alisisitiza Wakili Mbagwa.
Mshtakiwa wa kwanza, Simba alikiri kuwa kweli anamiliki akaunti hizo zilizotajwa katika benki hizo na kwamba Kisena aliingiza katika akaunti zake jumla ya Sh milioni 320 , kwa nyakati tofauti.
Hata hivyo alikana kutumia sehemu ya fefha hizo kwa ajili ya kununulia gari na kwamba fedha hizo hazikuwa sehemu ya malipo ya uuzwaji wa hisa za UDA.

“Si  kweli mheshimiwa hakimu , ni uzushi na uwongo kuwa hizo Sh milioni 320  zilizoingizwa katika akaunti zangu zilikuwa malipo ya awali au ya aina yoyote ya katika ununuzi wa hisa za UDA.”, alidai Idd Simba hata hivyo bila kufafanua kuwa zilikuwa ni za nini.

Pia Idd Simba alikiri kuwa kulikuwa na hisa 15 milioni za UDA na kwamba serikali ilikuwa ikimiliki asimilia 49 ya hisa hizo, lakini akasisitiza kuwa uuzwaji wa hisa hizo kwa Simon Group ulifuata utaratibu wa kawaida na kwamba  uamuzi wa kuuza hisa hizo haukutolewa na yeye na washtakiwa wenzake bali ulitolewa na Bodi nzima ya UDA.

Pia Simba akiri taarifa binafsi za utambulisho wake yakiwemo majina, vyeo  na akaunti mbalimbali anazozimiliki katika benki mbalimbali.
 
Washtakiwa wenzake pia walikiri maelezo ya utambulisho wao binafsi kama majina na nafasi zao kama watendaji wa UDA lakini wakakana mashtaka yanayowakabili.

Hakimu Mugeta aliairisha kesi hiyo hadi Kesi hiyo hadi Februari 4 na 5, mwaka huu, kesi hiyo itakapoanza rasmi kusikilizwa kwa mashahidi wa upande wa jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao.
 
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa,Januari 4 mwaka 2013

3 comments:

Anonymous said...

I all the timе emailed this web ѕіte post page to all my аsѕοciates, ѕince if liκe tо read it
аfteгωаrd my friends will tοo.
The Big Bang Theory Season 6 Episode 12 The Egg Salad Equivalency
Also visit my blog :: The Big Bang Theory Season 6 Episode 12 Free Stream

Anonymous said...

I feel this іѕ amοng the most vital information for
mе. And i'm happy reading your article. But want to observation on some basic issues, The website style is wonderful, the articles is truly nice : D. Good task, cheersElementary Season 1 Episode 11 Dirty Laundry
Take a look at my web blog Elementary Season 1 Episode 11 Free Stream

Anonymous said...

Hello, yup thiѕ piece οf wгitіng is in fact pleasant and I
hаve leaгned lоt of things from it on the
topic of blogging. thаnks.httρ://upсoming.

уahoo.сom/evеnt/10692582/IL/Chicago/Watch-CSI-Νеw-Yoгk-Ѕeason-9-Episodе-11-onlinе-CοmmаndΡ/Chicago-Theаtre/
Here is my webpage CSI: New York Season 9 Episode 11 Free Stream

Powered by Blogger.