RUFAA YA DPP V ZOMBE KUSIKILIZWA DECEMBA 11
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Rufani nchini
imepanga kuanza kusikiliza rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa
Mashtaka(DPP),Dk.Eliezer Feleshi ya kupinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar
es Salaam , ilimwachilia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es
Salaam,Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Abdallah Zombe na wenzake itaanza kusikilizwa Desemba 11 mwaka huu.
Kwa mujibu wa ratiba ya
vikao iliyotolewa na mahakama hiyo inaonyesha rufaa hiyo inayosubiriwa kwa
shauku kubwa na umma itaanza kusikilizwa kuanzia saa tatu asubuhi mahakamani
hapo jijini Dar es Salaam.
Aidha ratiba hiyo ya vikao
inaonyesha jopo la majaji watatu ambao ni Jaji William Mandia, Nathalia
Kimaro na Jaji Katherine Oriyo ndiyo wamepangwa kuikisiliza rufaa hiyo Na.
254/2009 iliyokatwa na DPP ,Dk.Feleshi Oktoba 6, 2009.
Ambapo katika rufaa hiyo
DPP ametoa sababu 11 za kukata rufaa ambapo alidai Jaji Massati alikosea
kisheria kuwaachiria huru washtakiwa na
kwamba anaiomba mahakama ya rufaa itengue hukumu ya Mahakama Kuu iliyotolewa na
Jaji Massati Agosti 17 mwaka 2009 ,
kwasababu ina mapungufu mengi ya kisheria na jaji huyo alijielekeza vibaya
katika kutoa hukumu ile iliyowaachilia huru washtakiwa.
Walikuwa wakidaiwa kuwa
kutenda makosa hayo tahere 14 Januari 2006, katika msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis,
Jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara hao ni
Sabinus Chigumbi, au Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe
pamoja na Juma Ndugu, dereva teksi.
Mbali na Zombe aliyekuwa
akitetewa na wakili wa kujitegemea Jerome Msemwa, washtakiwa wengine walikuwa
ni ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Noel Leonard, Konstebo
Jane Andrew, Koplo Nyangerela Moris, Konstebo Emanuel Mabula na Koplo Felix
Sedrick,
Wengine walikuwa ni
Konstebo Michael Shonza, Koplo Abeneth Salo, Koplo Rashid Lema (aliyefariki
kabla ya kujitetea), Koplo Rajabu Bakari na Koplo FestusGwabisabi.
2 comments:
I think this is one of the mοst importаnt infο foг mе.
And i аm glаd reading your artiсle.
But wannа remarκ on few general things, The ωeb site style is ideаl,
the aгticles is really excеllent : D. Good ϳоb,
cheerѕhttp://sоundclouԁ.cοm/usеr58513297/watch-criminal-mindѕ-season-8
my web site > Criminal Minds Season 8 Episode 8
I abѕolutely loѵe your site.. Pleasаnt colorѕ & themе.
Did you devеlop thiѕ ѕite уouгself?
Pleaѕe геply baсk as
I'm looking to create my very own blog and would love to know where you got this from or exactly what the theme is named. Kudos!Private Practice Season 6 Episode 7 The World According to Jake
my webpage: Private Practice Season 6 Episode 7 The World According to Jake
Post a Comment