HUKUMU YA KESI YA PONDA YAOTA MBAWA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, jana ilishindwa kutoa hukumu ya kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na wenzake 49 kwa maelezo kuwa hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Victoria Nongwa hayupo na wala hajaituma hukumu hiyo kwa uongozi wa mahakama.
Hakimu Mkazi Alocye Katemana ndiye aliyeairisha kesi hiyo ambapo alianza kwa kusema kesi hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutolewa hukumu, lakini hukumu hiyo haitatolewa kwasababu hakimu anayesikkiliza kesi hiyo hayupo na wala hajatuma hukumu ya kesi hiyo.
‘Kwa sababu hiyo naairisha kesi hii hadi Mei 2 itakapokuja kwaajili ya kutajwa na kwamba Mei 9 mwaka huu, itakuja kwaajili ya kutolewa hukumu na hivyo kuamuru mshitakiwa wa kwanza na watano(Ponda na Mukadamu Swalehe) kurudishwa rumande kwasababu hadi sasa Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP).Dk.Elizer Feleshi ajaondoa hati yake ya kuwafungia dhamana.
Mwandishi wa habari hizi ambaye alifika mahakamani hapo tangu saa moja asubuhi ,alishuhudia kundi la watu zaidi ya mia moja wakiwa wamesimama nje ya uzio wa mahakama hiyo karibu na ofisi ya Maktaba ya Taifa tayari wakisubiri kuingia ndani ya geti la mahakama hiyo kwaajili ya kukaguliwa kwa vifaa maalum na wanausalama ambapo hata hivyo waliruhusiwa na kuingia ndani ya viwanja vya mahakama, lakini ni wafuasi wachache ndiyo walioruhusiwa ndani ya chumba cha wazi Na. mbili cha mahakama hiyo kwaajili ya kusikiliza kesi hiyo.
Baada ya kuarishwa kesi hiyo askari magreza waliondoka na msafara wa magari yao ambao ulikuwa ukiongozwa na askari polisi waliokuwa wamevalia sare na wale ambao hawajavalia sare za jeshi hilo, na wakati wakitoka ndani ya viwanja hivyo tayari kwaajili ya kuelekea katika gereza la Segerea anapoishi Ponda na Mukadamu ,wafuasi hao walianza kupaza sauti huku wakimpungia mkono Ponda na kusema ‘ Takbirii Abkbaru ’.
Aprili
3 mwaka huu:Mawakili
wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma
Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya
maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone
washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.
Wakati
mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na
iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda makosa yanayowakabili na kwamba
upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.
Machi
21 mwaka huu;Sheik
Ponda, mshitakiwa wa tano Mukadamu Swaleh walijitetea.Na washitakiwa wenzake wa
nne nao walijitetea siku hiyo na hivyo kufanya jumla ya washitakiwa 48 wa kesi
hiyo kumaliza kutoa utetezi wao.Na siku hii ndipo upande wa utetezi walifunga
utetezi wao na Hakimu Nongwa aliipanga tarehe ya jana ndiyo angetoa hukumu ya
kesi hiyo.
Machi
4 mwaka huu: Hakimu
Nongwa atoa uamuzi wake ambapo aliwaona washitakiwa wote wana kesi ya kujibu na
akatupilia mbali hoja ya mawakili wa utetezi iliyokuwa ikidai kesi hiyo ni ya
madai na kwamba ifutwe.
Oktoba 18 mwaka jana, Ponda na wenzake walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza ambapo wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano na makosa hayo ni kama yafuatayo.
shitaka
la kwanza ni la kula njama kinyume na kifungu 384 cha Sheria ya Kanuni ya
Adhabu ya mwaka 2012,kwamba Oktoba 12 mwaka huu, huko eneo la Chang’ombe
Markasi washitakiwa wote walikula kwa nia ya kutenda kosa hilo.
Shitaka
la pili wakili Kweka alidai linawakabili washitakiwa wote ambalo ni la kuingia
kwa nguvu kwa nia ya kutenda kosa kinyume na kiufungu cha 85 na 35
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu na kwamba Oktoba 12 mwaka huu,
huko Chang’ombe Markasi , kwa jinai wasipokuwa na sababu za
msingi washitakiwa hao waliingia kwenye kiwanja kinachomilikiwa
kampuni ya AgriTanzania Ltd kwania ya kujimilikisha kiwanja
hicho isivyo halali.
Kabla
ya washitakiwa hakubali au kataa shitala hilo Ponda aliripoka na kusema yeye
anakanusha shitaka hilo na kwamba washitakiwa wenzake nao wanalikanusha shitaka
hilo,jambo ambalo lilikataliwa na Hakimu Sanga ambaye alimrisha kila mshitakiwa
ajibu shitaka hilo kwa kinywa chake ambapo kila mshitakiwa kwa kinywa chake
alikanusha shitaka hilo kinyume na alivyokuwa anataka Ponda iwe kwa yeye
kukanusha shitaka hilo kwa niaba ya wenzake.
Wakili
Kweka alilitaja shitaka la tatu kuwa ni kujimilikisha kiwanja kwa
jinai kinyume na kifungu cha 86 na 35 cha sheria hiyo na kwamba kati ya
Oktoba 12-16 mwaka huu huko Chang’ambe Markasi pasipo na uhalali
wowote washitakiwa wote katika hali iliyokuwa ikipelekea
uvunjifu wa amani walijimilikisha kwa nguvu ardhi ya
kampuni ya Agritanza Ltd.
Shitaka
la nne, wakili Kweka alidai ni la wizi ambalo ni kinyume na kifungu cha
258 cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, na kuwa kati ya Oktoba
12-16 mwaka huu, washitakiwa hao waliiba vifaa na malighafi,matofali
1500,nondo,Tani 36 za Kokoto vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh
59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza Ltd.
Aidha
shitaka la tano Kweka alidai ni la uchochezi ambalo linamkabili Sheikh Ponda
peke yake ambalo ni kinyume na kifungu cha 390 na 35 cha sheria
hiyo kwamba kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu katika eneo hilo la Chang’ombe
Markasi kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za
Kiislamu(T) aliwashawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao
kutenda makosa hayo na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
“Mheshimiwa
hakimu pamoja na kuwasomea mashitaka hayo ambayo yanadhamana kwa mujibu wa
sheria, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Elizer Feleshi kwa mkono wake
amenituma kuwasilisha kwaniaba yake mahakamani hapo hati ya kufunga dhamana kwa
mshitakiwa wa kwanza (Ponda) peke yake chini ya kifungu cha 148(4) cha
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2012’alidai wakili Kweka.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Aprili 18 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment