WALIOFANYA FUJO KATIKA KITUO CHA POLISI KAWE KORTINI
Na Happiness
Katabazi
WATU 12 jana
walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, kwa makosa
nane yakiwemo makosa ya kuaribu vioo vya magari ambavyo ni vielelezo na
kuwajeruhi kwa mawe askari polisi wa Kituo cha Polisi Kawe.
Mbele ya
Hakimu Mkazi Geni Dudu wakili Mwandamizi wa Serikali Tumaini Kweka alimtaja
mshitakiwa wa kwanza kuwa Alex Kalinga
na wenzake 12 ambapo miongoni mwao ni mwanamke mmoja aitwaye Eva Maheji.
Wakili Kweka
alilitaja kosa la kwanza kuwa ni la kula njama kutenda kosa kuwa Aprili 3 mwaka huko katika kituo cha
Polisi Kawe alishitakiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo.
Kweka alidai
kosala pili ni kufanya mkusanyiko husio halali ikiwa ni kwa washitakiwa hao
kutekeleza lengo moja ovu,walifanya mkusanyiko huo haramu ambayo ulisababisha
kuvunjika kwa amani.
Kosa la tatu
ni la kukaudi amri ya jeshi la polisi iliyokuwa ikiwataja watawanyike, kuwa
Aprili 3 mwaka huu, katika eneo hilo la Kituo cha Polisi Kawe jeshi hilo
lilitoa amri iliyowataka watawanyike lakini washitakiwa hao walikaidi.
Alilitaja
shitaka la nne ,tano, sita ni mashumbulio ya kudhuru mwili kwamba siku hiyo
washitakiwa waliwashambulia askari polisi waitwao Felex kwa kumpiga na jiwe kifuani, na pia
walimshambualia kwa kumpiga na jiwe usoni askari polisi aitwaye Harrison na
askari polisi aitwaye Aziz walimpiga na jiwe kichwani.
Wakati
shitaka la saba ni la kuharibu mali
ambapo siku hiyo washitakiwa hao walivunja kioo cha gari lenye namba za
usajili Na. T 212 APS Toyota Caridina chenye thamani ya Sh.400,000.
Kosa la nane
ni washitakiwa waliaribu kioo cha gari lenye Na. T 646 AZN Isuzu Troper chenye thamani ya Sh 400,000. Magari
yote hayo yaliyoaribiwa ni vielelezo vya kesi mbalimbali ambayo yameifadhiwa
katika Kituo hicho.
Hata hivyo
washitakiwa wamekana mashitaka yote na wakili Kweka amedai upelelezi wa kesi
hiyo haujakamilika na akaomba mahakamaiangalie mazingira na uzito wa kesi wakati inatoa dhamana na kwamba upande wa
jamhuri inaona kwasasa suo wakati mwafaka kwa mahakama hiyo kuwaoatia dhamana kwaajili
ya usalama wao kwaajili ya sababu za
upelelezi wa kesi hiyo.
Kwa upande
wao washitakiwa kila mmoja wao alikuwa akinyosha kidole juu, akiomba mahakama
impatie dhamana.
Lakini hata
hiyo Hakimu Dudu alisema mahakama yake inawanyima dhamana kwa muda hadi mangira ya kiusalama yatakapotengamaa na
akaiarisha kesi hiyo hadi Aprili 23 mwaka huu,itakapokuja kwaajili ya kutajwa
na akaamuru washitakiwa wote wapelekwe gerezani.
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com, Aprili 10 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment