MKENYA KORTINI KWA UTAKATISHAJI FEDHA
Na Happiness
Katabazi
RAIA wa
nchini Kenya Donibosco Ooga Bcha jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na makosa mawili likiwemo kosa la
utakatishaji fedha haramu zenye thamani ya Sh.bilioni 7.9.
Wakili Mwandamizi
wa Serikali Oswald Tibabyekomya mbele ya Hakimu Mkazi Emilius Mchauru alilitaja
kosa la kwanza kuwa ni la kula njama kutenda kosa la ambapo inadiwa kuwa kati ya Novemba 2009 na
Agosti 2010 huko Nairobi nchini Kenya, Arusha na Dar es Salaam,mshitakiwa huyo
alitenda kosa la utakashaji fedha haramu.
Wakili
Tibabyekomya alilitaja kosa la pili kuwa ni la utakajishaji fedha zenye thamani
ya Dola za Kimarekani Milioni 4.9 sawa
na Sh.bilioni 7.9 toka Nairobi kwenda
Arusha kuja Dar es Salaam.
Na kwamba
anadaiwa kuamisha kiasi hicho cha fedha kwa kutumia hundi yenye Na.
02J1036325000 inayomilikiwa na Moyale Prepious Germs Enterprices iliyopo benki
ya CRDB tawi la Meru mkoani Arusha.
“Na kisha anadiwa
kuamisha kutoka katika Tawi hilo la Arusha
kuja Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam kwania ya
kufanya utaratibu wa kuzitoa fedha hizo wakati akifahamu hundi
hiyo ilikuwa imegushiwa “alidai wakili huyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi
hiyo bado haujakamilika.
Hata hivyo
hakimu Mchauri alimtaka mshitakiwa huyo asijibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya
kusikiliza kesi hiyo na kwamba mahakama yenye mamlaka ya kuisikiliza ni
Mahakama Kuu na akaiarisha kesi hiyo Aprili 18 mwaka huu, itakapokuja kwaajili
ya kutajwa na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Aprili 11 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment