11 KORTINI KWA MAUAJI YA KUANGUKA KWA GHOROFA
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE
Mfanyabiashara Razah Hussein Razah na wenzake 10 jana walifikishwa katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na jumla ya makosa
24 ya kuua bila kukusudia.
Mbali na
Razah washitakiwa wengine ni Godluck Mbaga,Wilbroad Mugabisyo,Ibrahim
Kisoki,Mohamed Abdubakari,Charles Salu, Zonazea anage,Vedasto Ferand,Michael
Hemed Hemed,Albert Jones na Joseph Ringo ambao waliletwa jana saa nane mchana chini ya ulinzi mkali wa
wanausalama ambao walikuwa wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi
Ilala(RCO), Duwani Nyanda.
Mbele ya
Hakimu Mkazi Devotha Kisoka mawakili waandamizi wa serikali waliokuwa
wakiongozwa na Bernad Kongora, Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya, Peter Mahugo, Kinyeshi waliwasomea mashitaka hayo
kwa kupokezana.
Wakili
Kongora alidai mashitaka yote hayo 24 yanayowakabili washitakiwa wote
yanafanana na kwamba wanakabiliwa na makosa ya kuua bila kukusudia kinyume na
kifungu cha 195 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , kuwa mnano
Machi 29 mwaka huu huko katika eneo la Mtaa wa Indragand waliwaua watu 24 bila
kukusudia.
Hata hivyo
wakili Kongora aliwataka washitakiwa hao wajibu chochote kwakuwa mahakama hiyo
haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba mahakama yenye mamlaka ya
kusikiliza kesi hiyo ni Mahakama Kuu na kwamba upepelezi bado haujakamilika na
kwamba wanaomba mahakama isiwapatie dhamana kwasababu mahakama hiyo haina
mamlaka ya kuwapatia dhamana.
Hata hivyo
mawakili wa utetezi zaidi ya saba ambao Jerome Msemwa, Adronicus Byamungu,John
Mhozya waliomba mahakama hiyo iwapatie dhamana na washitakiwa wanao wadhamini
wakuaminika kwasababu tayari kuna maamuzi mbalimbali yalishatolewa na mahakama
ya Rufaa na mahakama Kuu katika kesi za makosa ya kujaribu kuua ,mahakama hizo
zilisema mahakama za chini zina mamlaka ya kutoa dhamana kwa kesi ambazo
zinafunguliwa kwanza mahakama ya chini na kisha zinakuja kuamishiwa mahakama
kuu kwaajili ya usikilizwaji.
Hata hivyo
mawakili wa serikali walipinga maombi hayo kwa maelezo kuwa maamuzi hayo ya
mahakama rufaa yalitolewa kwenye kesi ya kujaribu kuua wakati kesi
inayowakabili washitakiwa hao ni kuua bila kukusudia na kusisitiza kuwa
mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na hivyo haina mamlaka ya
kuwapatia dhamana.
“Mheshimiwa
hakimu sisi upande wa Jamhuri tunawasii
mawakili wa washitakiwa wawe watulivu na wavumilivu kwani kesi hii ndiyo kwanza
imefunguliwa leo, na upelelezi bado haujakamilika na sheria zilizotungwa na
bunge zipo wazi kabisa zinasema ni Mahakama Kuu peke yake ndiyo yenye mamlaka
ya kusikiliza kesi hii na si mahakama hii hivyo tunasisitiza kuwa mahakama hii
haina mamlaka ya kutoa dhamana’alidai wakili Kongora.
Itakumbukwa kuwa
Machi 29 mwaka huu, ghorofa mmoja lililokuwa linajengwa katika mtaa wa
Indragand lilianguka na kusababisha watu
idadi hiyo ya watu 24 kupoteza maisha.
Chanzo:Gazeti la
Tanzania Daima la Alhamisi, Aprili 4 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment