OMBI LA LWAKATARE KUSIKILIWA LEO MAHAKAMA KUU
Na Happiness
Katabazi
JAJI Lawrance Kaduri wa Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam,leo anatarajiwa kuanza
kusikiliza ombi Na. 14/2013,lilowasilishwa na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare na Ludovick
Joseph ),wanaokabiliwa na kesi ya tuhuma za ugaidi.
Lwakatare
anayetetewa na mawakili wa kujitegeema Tundu LIssu na Peter Kibatara , mawakili hao wanaomba
mahakama hiyo ifanyie marejeo wa majadala ya kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa
wa Machi 18 mwaka huu na Mkurugenzi wa Mashitaka,Dk.Eliezer
Feleshi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Lwakatare na Ludovick
Joseph mbele ya hakimu Emilius Mchauru
ambapo siku hiyo alisikiliza maombi
ya pande mbili.
Maombi ya
mawakili wa utetezi yaliomba washitakiwa wapewe dhamana wakati mawakili wakuu
wa serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo waliomba
mahakama isitoe dhamana kwasababu kesi makosa yanaoyoangukia katika sheria za
ugaidi ya mwaka 2002 hayana dhamana.
Ambapo siku
hiyo hakimu Mchauru aliairisha kesi hiyo hadi Machi 20 kwaajili ya kuja kutolea uamuzi wa maombi
hayo pamoja na maombi mengine lakini
hakimu huyo alijkuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwasababu Mkurugenzi
wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi amewasilisha hati ya kuwafutia kesi washitakiwa hao chini
ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2002
kwasababu hana haja ya kuendelea
kuwashitaki.
Lakini
dakika chache baada ya hakimu Mchauru kuwafutia kesi hiyo, wanausalama
waliwakamata tena washitakiwa hao na kisha kuwapandisha mahakamani mbele ya
Hakimu mwingine Alocye Katemana na wakili wa serikali Rweyongeza alianza kuwasomea mashitaka manne
mapya katika kesi mpya iliyopewa Na.6/2013 ambayo mashitaka ni yale yale yaliyokuwa kwenye hati ya mashitaka ya
awali iliyofutwa na DPP,ambapo Katemana
aliwataka washitakiwa wasijibu chochote na akaamuru waende gerezani na kesi
hiyo itakuja kutajwa tena Aprili 17 mwaka huu,kwa sababu jalada la kesi hiyo
lipo Mahakama Kuu.
Kwa mujibu
wa madai yao mawakili wa Lwakatare wanaomba Mahakama Kuu ipitie uamuzi wa DPP wa kuifuta hati ya awali ya mashitaka na
kisha kuwafungulia kesi upya washitakiwa hao wakati kesi hiyo ilikuwa imekuja
kwaajili ya mahakama kuitolea uamuzi lakini mahakama ikashindwa kutoa uamuzi
wake kwasababu DPP aliwasilisha hati ya kuifuta kesi hiyo.
Kosa
la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda
kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba
28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o
Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Denis Msaki
ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na
kifungu cha 227 cha sheria hiyo.
Wakili
Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa
ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili
ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na
kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo
washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la
kutaka kumteka Msaki kinyume na
kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya
Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
Shitaka
la tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya
Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa kupanga
kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki
kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.
Shitaka
la nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi
kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28
mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka
King’ong’o kwa makusudi aliliruhusu
kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka
nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com ; Facebook:
happy katabazi ;Aprili 15 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment