OMBI LA LWAKATARE KUSIKILIZWA APRILI 15
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA
Kuu Kanda ya Dar es Salaam, April 15 mwaka huu, itasikiliza ombi lilowasilisha
mbele yake na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo(Chadema), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph wanaokabiliwa na
makosa ya ugaidi liaomba mahakama hiyo ifanyie marejeo majalada ya kesi hiyo ya
msingi yaliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Kwa
mujibu wa mawakili wa Lwakatare Peter Kibatara aliliambia gazeti hili kuwa
tayari wameishapokea wito wa mahakama huu unaonyesha ni jaji Lawlence Kaduri
ndiye atasikiliza ombi hilo Aprili 15 mwaka huu, mahakamani hapo.
Machi
22 mwaka huu, mawakili wanaomtetea
Lwakatare,Peter Kibatara na Tundu Lissu waliwasilisha Mahakama Kuu Dar es Salaam, ombi namba 14 la
mwaka huu, la kuomba mahakama hiyo iitije majadala ya kesi tuhuma za ugaidi
zilizofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwaajili ya kuzifanyia
marejeo.
Kwa
mujibu wa kiapo kilichoapwa na wakili Kibatara, mawakili hao wanaomba mahakama
hiyo ifanyie marejeo wa majadala ya kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa wa
Machi 18 mwaka huu na Mkurugenzi wa Mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu dhidi ya Lwakatare na Ludovick Joseph mbele ya hakimu Emilius
Mchauru ambapo siku hiyo alisikiliza
maombi ya pande mbili.
Maombi
ya mawakili wa utetezi yaliomba washitakiwa wapewe dhamana wakati mawakili
wakuu wa serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo waliomba
mahakama isitoe dhamana kwasababu kesi makosa yanaoyoangukia katika sheria za
ugaidi ya mwaka 2002 hayana dhamana.
Ambapo
siku hiyo hakimu Mchauru aliairisha kesi hiyo hadi Machi 20 kwaajili ya kuja kutolea uamuzi wa maombi
hayo pamoja na maombi mengine lakini
hakimu huyo alijkuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwasababu Mkurugenzi
wa Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi
amewasilisha hati ya kuwafutia kesi
washitakiwa hao chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
Jinai ya mwaka 2002 kwasababu hana haja
ya kuendelea kuwashitaki.
Lakini
dakika chache baada ya hakimu Mchauru kuwafutia kesi hiyo, wanausalama
waliwakamata tena washitakiwa hao na kisha kuwapandisha mahakamani mbele ya
Hakimu mwingine Alocye Katemana na wakili wa serikali Rweyongeza alianza kuwasomea mashitaka manne
mapya katika kesi mpya iliyopewa Na.6/2013 ambayo mashitaka ni yale yale yaliyokuwa kwenye hati ya mashitaka ya
awali iliyofutwa na DPP,ambapo Katemana
aliwataka washitakiwa wasijibu chochote na akaamuru waende gerezani hadi Aprili
tatu.
Kwa
mujibu wa madai yao mawakili wa Lwakatare wanaomba Mahakama Kuu ipitie uamuzi
wa DPP wa kuifuta hati ya awali ya
mashitaka na kisha kuwafungulia kesi upya washitakiwa hao wakati kesi hiyo
ilikuwa imekuja kwaajili ya mahakama kuitolea uamuzi lakini mahakama ikashindwa
kutoa uamuzi wake kwasababu DPP aliwasilisha hati ya kuifuta kesi hiyo.
Kosa
la kwanza ambalo linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda
kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na kwamba mnamo Desemba
28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o
Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Denis Msaki
ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na
kifungu cha 227 cha sheria hiyo.
Wakili
Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa
ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili
ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na
kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo
washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la
kutaka kumteka Msaki kinyume na
kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya
Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
Shitaka
la tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya
Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa
kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria
ya Kuzuia Ugaidi.
Shitaka
la nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi
kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28
mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka
King’ong’o kwa makusudi aliliruhusu
kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka
nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.
No comments:
Post a Comment