CHE MUNDUGWAO ADAI ANATESEKA GEREZANI
Na Happiness
Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya wizi wa
paspoti inayomkabili msanii wa muziki wa asili nchini, Chingwele
Che Mundugwao na wenzake nane wanaokabiliwa na kesi ya wizi wa pasipoti 26
wamewasilisha taarifa ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa,inayoiomba Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es salaam,
iwaongezee siku 60 iliwaweze kuendelea kufanya upelelezi wao.
Mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo,
wakili wa serikali Adolph Mkini aliwasilisha ombi hilo jana asubuhi ambapo
alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwaajili ya kutajwa na
kwamba upande wa jamhuri unaombi la kuwasilisha hati iliyoletwa na RCO ya
kuiomba mahakama iwaongezee muda wa siku 60 kuanzia jana ili waweze kuendelea
kufanya upelelezi wa kesi hiyo.
Baada ya Wakili Mkini kumaliza
kuwasilisha ombi hilo, mshitakiwa Che Mundugwao alianza kuwasilisha kilio chake
kuwa jela ni sehemu mbaya sana na kwamba wanavyozidi kukaa gerezani wanateseka
pia wanaomba mahakama iwapatie dhamana kama ilivyomoatia dhamana Wilfred
Lwakate wa Chadema na kwamba anaomba mahakama imruhusu wakili huyo wa serikali
waongozane naye waende naye gerezani ili akashuhudie wanavyoteseka na maisha ya
gerezani.
Hata hivyo
Hakimu Fimbo alikubaliana na ombi hilo la RCO la kuomba waongezewe muda wa siku
60 na akasema mahakama yake haiwezi kutoa masharti ya dhamana kwa kesi
hiyo kwani ni MKurugenzi wa
Mashitaka(DPP), Dk.Eliezer Feleshi ndiye aliyewasilisha hati ya kuwafungia
dhamana na moja ya sababu iliyotajwa na DPP ya kuwafungia dhamana ni kwamba bado paspoti 22 hazijapatikana na kuwa
bado washitakiwa wengine hawajakamatwa ili waje kuunganishwa kesi hiyo na
ninawashauri washitakiwa mistake kufananisha mazingira ya kesi hii sawa na kesi
nyingine kama ya Lwakatare, mazingira na mashitaka yanayowakabili nyie na
Lwakatare ni tofauti..
“Kwa sababu
hadi sasa DPP bado hajaiondoa hiyo hati yake ya kuwafungia nyie washitakiwa
dhamana, mahakama yangu kisheria imefungwa mikono haiwezi kuwapatia dhamana
hadi pale siku DPP atakapoamua kuindoa hati yake hivyo naamuru mrejeshwe
rumande hadi Agosti 19 mwaka huu, kesi hii itakapokuja kwaajili ya kutajwa’alisema
Hakimu Fimbo.
Mbali na Che Mundugwao washitakiwa
wengine ni wahudumu wa Idara ya uhamiaji Adam
Athuman na Abdallah Salehe , Rajab Momba
na Haji Mshamu
Raia wa Uingereza Ahsan Iqbal au Ali
Patel, Ofisa Ugavi wa Idara ya Uhamiaji Shemweta Kiluwasha, Injinia
Keneth Pius wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji na mfanyabiashara Ally
Jabir.
Juni 3 mwaka huu, Chemundugwao na
wenzake walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa
mbalimbali yakiwemo kosa la wizi wa paspoti 26, ambapo hata hivyo DPP
aliwasilisha hati ya kuwafungia dhamana ambapo hadi sasa wapo gerezani.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Agosti 6 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment