URANIUM YAWAPELEKA JELA
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imewahukumu watu wawili kwenda jela miaka
mitatu kwa kosa la kukutwa wakilimi madini aina ya Uranium Kg. 6.5.
Hukumu hiyo
ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Gene Dudu ambaye aliwataja washitakiwa waliokuwa
wakikabiliwa na kesi hiyo ya mwaka 2012 ni Duncan Mwananemela(41) na Silvia
Mwemis (42) ambapo Julai 30 mwaka jana
wakili wa serikali alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na kosa la kukutwa
wakimiliki madini yenye mionzi mikali
kinyume na kifungu cha 11(1),(2) cha Sheria
Na.7 ya Nguvu za
Atomiki ya mwaka 2003.
Hakimu Dudu
alisema ili kuthibitisha kesi hiyo upande wa jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na
wakili wa serikali Charles Anindo ulileta mashahidi wa nne ambao wameweza
kuthibitisha kesi yao na kwamba mahakama yake imefikia uamuzi wa kuwakuta na
hatia wa kosa hilo washitakiwa wote wawili.
Na katika
ushahidi wa jamhuri ulionyesha kuwa baada ya kupimwa madini yenye mionzi mikali
waliyokutwa nayo washitakiwa ambayo walikuwa wameyaifadhi kwenye vyumba
wanavyolala majumbani kwao, ni Uranium
na kwamba kisayansi madini
hayatakiwi kuwekwa karibu na makazi yanayoishi binadamu kwani madini hayo ya madhara makubwa
ambayo yakiwekwa katika makazi ya watu
yanasababisha ulemavu, yanaaribu mfumo
wa uzazi,kuaribu Ini na Figo na kwamba kama yatalazimika madini hayo kuwekwa
kwa watu basi madini hayo yanatakiwa yafungwe kitaalamu
ambapo licha yakuwa yamefungwa kitaalam madhara yatokayo na mionzi hiyo
iliyofungwa kitaalamu na kukaa kwenye makazi wanayoshi binadamu yanaweza
kujitoka miaka mitatu baadaye.
“Nawahukumu
kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh.milioni tatu kwani sheria ya
Nguvu ya Atomiki inatoa adhabu hiyo….lakini mahakama hii imewatizama
washitakiwa wote na imeona hamna huwezo wa kulipa fidia hiyo na kwa mujibu wa
utetezi wa washitakiwa walidai kuwa walikuwa hawaelewi na madhara yatokanayo na
mtu kimiliki madini hayo ya kemikali ;
‘Hivyo basi
mahakama hii licha imewahukumu kwenda jela miaka mitatu pia inaamuru
washitakiwa waende gerezani kwa siku 14 kuanzia leo na katika kipindi cha siku
hiyo watakuwa chini ya ungalizi wa maofisa wa Ustawi wa jamii ambao watakuwa
wakiwaangalia kama wanatabia njema na kama wataonyesha tabia njema mahakama
hiyo itakuja kuwabadilishia adhabu ambapo itakuja kuwapatia adhabu ya kuja
kutumikia kifungo cha nje”alisema Hakimu Dudu.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Agosti 16 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment