ALEX MASSAWE AFUNGULIA KESI YA KUGHUSHI
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imetoa hati ya kukamatwa na kurejeshwa nchini
mfanyabiashara maarufu nchini Alex
Siliyamala Massawe ili aje kukabiliana na kesi yake mpya ya kughushi nyaraka za
umiliki wa ardhi na kutoa taarifa za uongo.
Amri hiyo
imetolewa na Hakimu Mkazi Gene Dudu muda mfupi baada ya wakili Mwandamizi wa
serikali Tumaini Kweka kuwasilisha ombi hilo mahakamani na kuiarifu mahakama
kuwa upande wa jamhuri umemfungulia kesi Massawe na.150/2013 ya kughushi hati za
umiliki wa ardhi na kutoa nyaraka za uongo mahakamani hapo na kumsomea
mashashitaka Massawe ambaye anashikiliwa na Askari wa Interpol Dubai bila ya
Massawe kuwepo mahakamani hapo .
Hakimu Dudu
alisema anakubaliana na ombi hilo la wakili Kweka na kwamba mahakama yake
imetoa amri ya kukamatwa kwa Masawe kokote alipo na arejeshwe nchini ili aje
akabiliane na kesi yake hiyo mpya iliyofunguliwa mahakamani hapo.
Aidha Hakimu
Dudu alisema pia anakubaliana na ombi la wakili Kweka lilokuwa linaiomba
mahakama hiyo itamke majina sahihi yanayotumiwa na Massawe hata kama
kule Dubai anakoshikiliwa na
askari wa Interpol anatumia majina mengi, ambapo hakimu Dudu alisema
majina halali ya Massawe ni Alex Siliyamala Massawe ambayo ndiyo yaliyoandikwa
kwenye hati ya mashitaka ya kesi hiyo Na.150 ya mwaka huu.
Hivi
karibuni vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Interpol cha Jeshi la Polisi
hapa nchini , Babile alithibitishia vyombo vya habari kuwa Massawe amekamatwa
na askari wa Interol huko Dubai kwa tuhuma mbalimbali.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Agosti 24 mwaka 2013
No comments:
Post a Comment