JELA MIAKA MITANO KWA KUIBA KWENYE AKAUNTI YA JESHI LA POLISI
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemhukumu Afisa wa Jeshi la
Polisi Edna Kadogo na wenzake kifungo
cha miaka mitano jela baada ya kuwakuta na hatia ya makosa ya kula njama na
kuibia Benki ya NMB jumla ya Sh. Milioni 330.
Mbali Edna wengine waliotiwa hatiani
katika kesi hiyo iliyokuwa na jumla ya washitakiwa tisa ni Adelaida Lwekoramu,
na
Joshua Joshua Aseno Onditi Joshua Aseno
Onditi washitakiwa wengine sita
kuachiriwa huru.
Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu
Mkazi Gene Dudu ambaye alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa katika jitihada za
kuthibitisha kesi yao upande wa jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na wakili wa
serikali na mahakama hiyo baada ya kuona
upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yake dhidi ya washitakiwa hao
sita ambao ni Vedastus Limbu Mafuru,
Kennedy Agumba Achayo
Luciana Vedastus Limbu,
Agnes Robert Maro,
Mkika Gideon Nyasebwa na.
Amos Kabisi Hangaya,
Vedastus Limbu Mafuru,
Kennedy Agumba Achayo
Luciana Vedastus Limbu,
Agnes Robert Maro,
Mkika Gideon Nyasebwa na.
Amos Kabisi Hangaya,
ila imeweza kuthibitisha kesi yake dhidi ya
washitakiwa hao watatu na washitakiwa wote walikuwa wakitetewa na mawakili wa
kujitegemea Karegero Karegero na Ambokile Mwakaje.
Hakimu
Dudu alisema kesi hiyo ilikuwa na jumla ya mashahidi 21 wa upande wa jamhuri na
mashahidi 10 wa upande wa utetezi mashitaka matatu ambayo ni kula njama,
kughushi na wizi wa sh.milioni 330 ambapo ambapo alisema shitaka la kwanza la kula njama
na shitaka la tatu la wizi wa kiasi hicho cha fedha upande wa jamhuru umeweza
kuyathibitisha na kosa la kughushi, limeshindwa kuthibitika.
“Kwa
sababu hiyo mahakama hii ina wahukumu washitakiwa hao watatu katika kosa la kwanza la kula njama kwenda
jela mwaka mmoja, na katika kosa la tatu la wizi watakwenda jela miaka mitano
ili iwe fundisho kwa watu wengine kwani makosa ya wizi wa fedha kwa njia ya
mtandao yameanza kushamiri na kwamba anaukataa utetezi wa mwisho wa washitakiwa
hao watatu ambao waliomba wapunguziwe adhabu kwasababu wanafamili kubwa zinategemea
na kwamba sababu hiyo haiwezi kuishawishi mahakama iwapunguzie adhabu kwasababu
mimi binafsi naamini kama mtu anafamilia kubwa inamtegemea basi mtu huyo
anapaswa aepuke kutenda makosa ya jinai”alisema Hakimu Dudu.
Mwaka 2010 ilidaiwa na upande wa
jamhuri kuwa washitakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ya Na. 40/2010 kuwa
wanakabiliwa na kosa la kula njama, kughushi na wizi wa kiasi hicho cha
fedha kwenye akaunti inayomilikiwa na Jeshi la Polisi inayotambulika kwa
jina la Police Retention Collection Account No. 2011000015 kwenye benki ya NMB
Meatu.
Washtakiwa baadhi yao walikuwa
wafanyakazi wa NMB Meatu Tawi la Mwanhuzi na wengine walikuw
wafanyabiashara.
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com, Jumanne ,Agosti 6 mwaka 2013
No comments:
Post a Comment