PONDA ATOLEWA WODINI,APELEKWA GEREZA LA SEGEREA
Na Happiness
Katabazi
JESHI la Polisi na Jeshi la Magereza yamemwondoa hospitalini kimyakimya Katibu wa Taasisi na
Jumuiya za Kiislam, Sheikh Ponda Isa Ponda, na kumpeleka katika gereza
la Segerea bila ndugu zake kuwa na taarifa.
Wakili wa
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54)
ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo
mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Nassor Jumaa, ameliambia gazeti
hili jana saa saba mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Dar es Salaam, kuwa amesikitishwa na
hatua ya vyombo vya dola jana asubuhi
kumuondoa Ponda aliyekuwa amelazwa
katika wodi ya Kitengo cha Taasisi ya
Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu(MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha
kumwamishia katika gereza la Segerea.
Wakili Jumaa
alisema amesikitisha na kitendo hicho kwani hakimu Hellen Riwa juzi muda mfupi
baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea shitaka
Ponda, hakimu Liwa alitoa amri ya Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi lakini
cha kushangaza leo(jana),wanausalama wamemto wodi na kumpeleka katika gereza la
Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake
itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado
haujakamilika.
“Kwa kweli
kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana ….ila tunatafakari ni hatua
gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni’alisema wakili Jumaa.
Hata
hivyo baadhi ya maofisa wa Jeshi la
Magereza walilithibitishia gazeti hili kuwa Ponda amepelekwa rumande ya gereza
la Segerea na kudai kuwa wao walikua ni miongoni mwa waliotumwa kwenda kumtoa
wodini mshitakiwa huyo(Ponda), na kisha kiumpeleka gereza la Segerea.
Agosti 14
mwaka huu, saa kumi jioni Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliamia katika wodi
hiyo ya MOI na wakili wa serikali Tumaini Kweka alimsomea shitaka Ponda ambaye
anakabiliwa na kesi hiyo ya Jinai Na.144 ya mwaka huu.
Wakili Kweka
alidai mshitakiwa huyo anakabiliwa na kosa moja ambalo ni uchochezi kuwa Juni
2 hadi Agosti 11 mwaka huu, katika
maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akijifanya yeye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania,
aliwashawishi waumini wake katika maeneo hayo kutenda makosa ya jinai,
ikiwemo kosa la kutoa lugha ya kudhalilisha dhidi ya viongozi wa serikali . kutoa
maneno ambayo yalikuwa na lengo ya
kuamsha hisia na mawazo mabaya ya kidini
na aliwashawishi wafuasi wake
kufanya mikusanyiko,maandamano haramu mkinyume
na kifungu cha 390 na 35 cha Sheria ya
Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
Baada ya
wakili Kweka kumaliza kumsomea shitaka hilo,hakimu Riwa alitoa amri iliyotaka
Ponda aendelee kukaa chini ya ulinzi wa vyombo vya ulinzi.
Mei 9 mwaka
huu, aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa
alimfunga Ponda kifungo cha mwaka mmoja
jela baada ya kumkuta na hatia katika kosa moja kati ya matano yaliyokuwa
yakimkabilia mbapo kosa alilomtia nalo hatiani ni kosa la kuingia kwa jinai kinyume
na kifungu cha 85 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, katika kiwanja
cha Ch’angombe Marks.
Oktoba 18
mwaka jana, Ponda na wenzie 49 walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza
wakikabiliwa na makosa matano, kosa la kwanza ni la kula njama, kujimilikisha
mali, kuingia kwa jinai katika kiwanja cha Chan’ombe Markas,wizi wa malighafi
zenye thamani ya Sh. Milioni 59 na kosa la uchochezi ambapo katika kesi hiyo
Jamhuri ilikuwa ikiwakilishwa na serikali Tumaini Kweka na hakimu Nongwa akitoa
hukumu yake alisema anawaachiria huru washitakiwa 49 kwasababu jamhuri wameshindwa kuthibitisha
kesi dhidi yao na kwamba anamtia hatiani Ponda kwa kosa moja tu la kuingia kwa jinai na kwamba na
anamuachiria huru katika makosa manne yaliyosalia kwasababu pia jamhuri
ilishindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya Ponda.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Agosti 16 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment