MHARIRI KORTINI KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Na Happiness
Katabazi
MHARIRI wa
Habari wa Gazeti la Maua linalotolewa na
kampuni ya Hamkani Publisher Company Limited, Ibrahim Katemi Kadiro (36) jana
alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala Dar es Salaam, akikabiliwa na
makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa ya Dola za Kimarekani 6,700.
Wakili wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Leonard Swai mbele ya Hakimu Janeth
Kaluyenda alidai mshitakiwa ana kabiliwa na jumla ya makosa mawili.
Wakili Swai
alilitaja kosa la kwanza kuwa ni kuomba rushwa na kuwa Julai 31 mwaka huu,
katika Mtaa wa Samora katika jengo la
Habour View Tower , Kadiro akiwa ni wadhifa wa mhariri msaidizi wa Hamkani Publisher inayochapisha gazeti la Maua alimuomba rushwa
sh.milioni 12 kutoka kwa Costa
Ginakopolous ili asichapishe habari mbaya inayohusu biashara biashara zinazofanywa na
kampuni ya Costa.
Wakili Swai
alilitaja kosa la pili kuwa ni la kupokea rushwa ambalo alilitenda Agosti Mosi mwaka huu, ambapo alipokea dola
za Kimarekani 6,700 kutoka kwa
Costa ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa
Kampuni ya Thinany Entertaiment ili asiweze kuichapisha habari ya tuhuma zinazoikabili
kampuni hiyo ambayo Costa ana mahusiano nayo ya kibiashara.
Hata hivyo
mshitakiwa huyo alikana mashitaka na Hakimu Kaluyenda alisema makosa
yanayomkabili mshitakiwa huyo yana dhamana kwa mujibu wa sheria ila hawezi
kumpatia masharti ya dhamana kwa siku ya jana kwasababu yeye siyo hakimu
aliyepangwa kusikilizwa kesi hiyo kwani hakimu aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo
ni Joyce Minde ambaye yupo nje ya ofisi na hivyo akaiarisha kesi hiyo hadi Agosti
16 mwaka huu, na akaamuru mshitakiwa apelekwe gerezani.
Wakati huo huo, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Ge
nu Dudu
ameiarisha kesi ya kujipatia kujipatia kofia,fulana zenye jumla
ya thamani ya shilingi milioni 74.9 kwa njia ya udanganyifu
inayomkabili waziri wa zamani na Kada wa Cha cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema),Arcado Ntagazwa na wenzake hadi Agosti 12,13 na 14.Kesi hiyo jana
ilikuja kwaajili Ntagazwa kuanza kujitetea.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Agosti 6 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment