RAIS MKAPA AZINDUA THE GLOBAL BUSSINESS ROUNDTABLE
Na Happiness
Katabazi
RAIS Mstaafu
Benjamin Mkapa amewaasa wanataaluma, wafanyabiashara na wote wanaomwamini
Mwenyezi Mungu hapa nchini kuketi pamoja
na kujadiliana na kushauri ni mbinu gani zitumike ili ziweze kuwainua
wafanyabiashara wadogo hususani katika sekta ya Kilimo.
Rais Mkapa
alitoa rai hiyo juzi usiku wakati alipokuwa anazindua rasmi utekelezwaji wa
kuanza kutumika kwa taasisi ya The Global Bussiness Roundtable (GBR) yenye
makao makao makuu yake nchini Afrika Kusini, hapa nchini ambapo iliudhuliwa na viongozi wa kiserikali, dini,wajasiliamali,
majaji, wasomi wa taaluma mbalimbali na wafanyabiashara.
Rais Mkapa
alisema uzinduzi huo GBR ambayo ni taasisi
ya Kiikristo ambayo yenye lengo la kuwaunganisha binadamu wote wanao amini
katika Mwenyezi Mungu ambao ni wasomi wa
taaluma mbalimbali, wafanyabiashara,serikali katika mataifa mbalimbali kuketi
pamoja na kwamba watumia fursa na rasilimali walizopewa na Mwenyezi Mungu na
taaluma zao waakikishe wanaweza kuleta maendeleo katika mataifa yao.
“Leo ni siku
muhimu kwa Tanzania kwani Tanzania na leo imejiunga na kuanza kufanyakazi na
GBR ambayo moja ya malengo yake ni
kuwaunganisha watu wote wanaomwamini Mwenyezi Mungu na ambao wanataaluma zao na
wafanyabaishara kuungana pamoja kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo ya
kiuchumi wao wenyewe na mataifa yao….lakini mimi napenda niseme kuwa nimefarijika na ujio wa GBR na niwaombe
washiriki wote mtaoshiriki katika mkutano huu mjadili na muanishe ni mbinu gani
zitumike kuinua hasa sekta ya kilimo
kwani kilimo ni biashara inayokuwa na
leo hii inaitaji wale wote wanaofanyabiashara katika sekta hiyo waweze
na mbinu za kisasa,mitaji ya kueleweka na waweze kuuza bidhaa zao zinazotokana
na kilimo kwa ngazi ya kimatifa”alisema Rais Mkapa.
Kwa upande
wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Profesa Costa Mahalu alisema kwanza inatakiwa binadamu wote
tupendane kama tunavyompenda mwenyezi Mungu na kwamba uzinduzi wa GBR hapa
nchini ,ambayo taasisi hiyo ina matawi
yake nchi 12 sasa kutawasaidia kuwaunganisha pamoja watanzania na mataifa
mengine kuweza kutumia rasilimali zilizowekwa na Mungu kwenye ardhi za nchi zao
kuweza kusaidiana ili wote waweze kufikia
ngazi ya juu ya maendeleo kwani Mungu amependi watu wake waishi maisha
ya ufukara.
Naye Balozi
wa Heshima nchini Malawi ambaye ni Mkurugenzi Mstaafu wa Kituo cha Uwekezaji
Nchini(TIC), Emmanuel Ole Naiko alisema
uwekezaji unaweza kufanywa na mtu yoyote yule na kwamba ujio wa GBR hapa
nchini, ni faida kubwa kwa watanzania kuweza kuungana na mataifa mengine
kujiletea maendeleo na kukuza uchumi wa biashara zao.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamis, Agosti 15 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment