HAKIMU AKWAMISHA KESI YA JEETU
Na Happiness Katabazi
KESI ya wizi wa sh bilioni 7.9 inayomkabili mfanyabiashara maarufu Jayantkumar Chandubhai Patel maarufu ‘Jeetu Patel na wenzake wawili, jana ilishindwa kuanza kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,kwasababu kutotimia kwa koramu ya mahakimu wakazi wanasikiliza kesi hiyo.
Mbali na Jeetu washitakiwa wengine ni Devendra Patel na Amin Nandy wanaotetewa na Mabere Marando na Kamala.Ambapo awali Wakili wa serikali Vitalis Timon aliyekuwa akisaidiana na Oswald Tibabyekoma waliambia mahakama kuwa wapo tayari kwaajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Kiongozi wa jopo Rwaichi Meela aliyekuwa akisaidiana na Grace Mwakipesile alisema jana kesi ambayo kwa mujibu wa ratiba ilikuwa imepangwa kuanza kusikilizwa haitaweza kusikilizwa kwa sababu ya mwanajopo mmoja John Kahyoza kuwa safari ya kikazi nje ya Dar es Salaam na kwamba anatarajiwa kurejea Jumatatu ijayo.
Meela alisema kuhusu ombi la mshitakiwa wa tatu Amit Nandy lakutaka aruhusiwe kwenda India kumsindikiza mke wake kwaajili ya kutibiwa, alisema wameshindwa kulitolea maamuzi na kwamba watalitolea maamuzi Agosti 10 mwaka huu, kwakuwa Kahyoza atakuwa ameisharudi jijini.
Novemba mwaka jana , ilidaiwa mahakamani hapo kuwa kati ya Agosti na Desemba 2005 ndani ya jijini la Dar es Salaam, washitakiwa hao waligushi nyaraka mbalimbali na zilizoonyesha kampuni yao ya Bencon International Limited imepewa idhini ya kurithi deni la kampuni ya Marubeni Corporation ya Japan na kufanikiwa kuiba sh 7,962,978,372.48 mali ya Benki Kuu ya Tanzania.
Wakati huo huo, Hakimu Mkazi Waliarwande Lema aliairisha kesi ya wizi wa bilioni 14 mali ya benki ya Bacralsy inayowakabili raia wawili wa Burgalia wawili, Nedkolazarous’ Standaev (35) na Stela Peteva Nedelcheva (23) hadi Agosti 13 mwaka huu, atakapokuja kutoa uamuzi wa washitakiwa wapate dhamana au la.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Agosti 4,2009
.

No comments:
Post a Comment