MARANDA,FARIJALA WAHUKUMIWA TENA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam, imemhukumu kwenda jela miaka miwili Kada wa Chama cha
Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na wenzake
waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kughushi,na kuisababishia serikali
hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya
Tanzania .
Sambamba na hilo jana Maranda
aligeuka mbogo na kabla ya jopo la majaji kuingia ndani ya ukumbi namba moja
kutoa hukumu dhidi yake, kwa kuwatolea lugha za vitisho wapiga picha wa
magazeti mbalimbali waliokuwa wakitaka kumpiga picha akiwa amekaa ndani ya chumba
cha mahakama kuwa amechoshwa na wapiga picha hao na kwamba hataki kupigwa picha
na endapo mpiga picha atampiga picha basi angemfunza adabu na kwamba yeye
haogopi tena kesi, na kwamba kukaa jela mungu amemuandikia na akiwa chini ya
ulinzi wa askari Polisi na Magereza Maranda aliamka kwenye kiti alichokuwa
ameketi na kuwafuata wapiga picha na kuanza kukagua kamera ya mpiga picha mmoja
kama endapo alikuwa amempiga picha na wakati akifanya hayo wanausalama hao
walikuwa wakimwangalia hali
iliyosababisha wapiga picha hao kuingiwa na woga na kushindwa kumpiga picha
akiwa ameketi ndani ya chumba cha mahakama.
Hukumu hiyo ya ilianza
kusomewa jana saa 8 hadi saa 11:56 jioni na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo
Ilvin Mugeta kwaniaba ya wanajopo wenzie Jaji Samuel Karua na Beatrice Mutungi
ambao walisema washitakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa sita ambayo ni kula
njama kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kughushi jina la biashara la
kampuni feki ya Lakshmil Textile Mills
Co Ltd ya India na hati ya kuamisha deni
iliyonyesha kampuni ya Maranda na Farijala ya Mibare Farm imepewa idhini ya
kudai la kampuni hiyo ya India katika BoT , kuwasilisha nyaraka zilizogushiwa katika
Benki ya Afrika na Benki Kuu ambazo zilionyesha nyaraka hizo zilikuwa
zimetolewa na BRELA,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kujipatia
ingizo toka BoT na kuisababishia BoT
hasara ya Sh bilioni 3.8 ambapo kosa hilo la sita lilikuwa likiwakabili maofisa
wa BoT ambao ni mshtakiwa wa 4,5 na 6 ambao ni (Iman Mwakosya, Ester Komu na
Kaimu Katibu BoT,Sophia Lalika ambao walikuwa wakitetewa na Richard Rweyongeza
na Majura Magafu na Ademba Agomba.
Hakimu Mugeta akiisoma hukumu
hiyo alisema mahakama imefikia uamuzi wa kulifuta kosa la tano ambalo ni la
kujipatia ingizo ambalo linamkabili mshtakiwa 1,2,3 ambao ni Farijala Hussein,
Rajabu Maranda na Ajay Somai kwasababu upande wa jamhuri umefanya makosa ya
kujumuisha kiwango cha fedha wanachowatuhumiwa kujipatia na kwamba mahakama
imelifuta kosa hilo na pia imewaachilia huru washtakiwa wote katika kosa la
kwanza la kula njama kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kosa
hilo.
Hakimu Mugeta alisema hata
hivyo upande wa Jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali
Oswald Tibabyekomya, Shadrack Kimaro, Tumaini Kweka umeweza kuthibitisha shtaka
la kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kuwasilisha nyaraka
zilizoghushiwa na kuisababishia serikali hasara na kwamba mashahidi wote saba
na vielelezo vya upande wa jamhuri vimeweza
kuishawishi mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa makosa hayo yaliyothibitishwa na
upande wa jamhuri.
Alisema katika kosa la pili,
mahakama hiyo imemtia hatiani Farijala peke yake na kwamba atatumikia adhabu
kifungo cha jela miaka mitatu jela, kosa la tatu ni Maranda na Farijala wametiwa hatiani na
watatumikia adhabu ya miaka miwili jela,na kosa la nne mahakama imemtia hatiani
Farijala, Maranda na Ajay Somai ambao watakwenda jela miaka miwili na kosa la
sita ni la kusababisha hasara ambapo mahakam imewatia hatia maofisa hao wa BoT,
Mwakosya, Komu na Lalika ambapo watalipa
faidi ya Sh.milioni tano kila mmoja na endapo watashindwa watakwenda jela miaka
mitatu.
Aidha Hakimu Mugeta alisema
mahakama yake imesikiliza ombi la wakili Mwandamizi wa serikali Kimaro ambaye
alitaka mahakama hiyo iwaamuru washitakiwa warejeshe serikalini kiasi cha fedha
ambacho serikali imepata hasara lakini imekubaliana na hoja wakili wa utetezi
Majura Magafu ambayo ilidai kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaonyesha
maofisa wa BoT walinufaika na kiasi hicho cha fedha ila kuna ushahidi
unaonyesha Maranda, farijala na Somai walinufaika na kiasi hicho cha fedha.
“Kwa sababu hiyo mahakama hiyo inamwamuru Farijala kuilipa
serikali fidia ya Sh 82,956,400, Maranda alipe Sh.616,443,600.10 na Somai alipe
Sh milioni 400 na endapo watashindwa kuilipa serikali fidia hiyo basi mali zao
zitakamatwa na kuongeza kuwa adhabu hiyo washtakiwa wataanza kuitumikia kuanzia
jana’alisema Mugeta hukumu washtakiwa hao wakilekwa na machozi kizimbani.
Hii ni kesi ya tatu kati ya
11 za wizi wa fedha za EPA zilizofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP),
Novemba 2008 zilizokwisha tolewa hukumu dhidi
ya washtakiwa mbalimbali ,kutolewa hukumu.Hukumu kwanza ni kesi ya jinai
Na.1161/2008 iliyokuwa ikimkabili Maranda na Farijala ya wizi wa sh bilioni 1.8
ambapo ilitolewa hukumu Mei mwaka jana, ambapo walikutwa na hatia na kuhukumiwa
kifungo cha miaka mitano jela na kesi nyingine ya EPA ni jinai Na. 1163/2008
ambapo Maranda na Farijala Mei mwaka
huu, walitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kwenda jela miaka mitatu na
hukumu nyingine ni kesi hii Na.1164/2008
ambayo ilitolewa hukumu jana na washtakiwa wakapatiakana na hatia.Kwa
hiyo hivi sasa Maranda atabakia akikabiliwa na kesi nyingine mbili za EPA na
Farijala atabakiwa akikabiliwa na kesi moja ya EPA ambazo bado hazijatolewa
hukumu.
Baada ya Hakimu Mugeta
kumaliza kutoa hukumu hiyo saa 11:56 jioni Mwakosyi,Komu na Lalika walishindwa
kulipa kiasi cha fidia walichoamriwa na mahakama walipe hivyo wakaungana na
Maranda na Farijala kwenda gerezani.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 23 mwaka 2012.
2 comments:
Τoԁay, I went to the beachfront with my kiԁs.
I found a seа ѕhell and gavе
it to my 4 year olԁ daughtеr and said "You can hear the ocean if you put this to your ear." Ѕhe placеd the ѕhell to
her ear and ѕcгeamed. There was a hermіt crab inside and it pinched her eаr.
She never wаnts to go bacκ! LoL I κnow this is entirely off topic but I had to tell someone!
http://wωw.discogs.сom/groups/topic/352280
Also visit my blog - Fun Size Movie Online
Нi there! Quіck questіοn that's entirely off topic. Do you know how to make your site mobile friendly? My weblog looks weird when browsing from my iphone. I'm trуіng to find a theme or plugin
that might be ablе tο resolvе this problem.
If you have anу suggeѕtiοnѕ, please share.
Thаnks!Wreck-It Ralph HD Free Streaming
Also see my web site :: Wreck-It Ralph HD Free Streaming
Post a Comment