Header Ads

MARANDA,FARIJALA WAHUKUMIWA TENA



Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, imemhukumu kwenda jela miaka miwili Kada wa Chama cha Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na wenzake  waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kughushi,na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3.8 katika Akaunti ya Madeni ya Nje katika Benki Kuu ya Tanzania .

Sambamba na hilo jana Maranda aligeuka mbogo na kabla ya jopo la majaji kuingia ndani ya ukumbi namba moja kutoa hukumu dhidi yake, kwa kuwatolea lugha za vitisho wapiga picha wa magazeti mbalimbali waliokuwa wakitaka kumpiga picha akiwa amekaa ndani ya chumba cha mahakama kuwa amechoshwa na wapiga picha hao na kwamba hataki kupigwa picha na endapo mpiga picha atampiga picha basi angemfunza adabu na kwamba yeye haogopi tena kesi, na kwamba kukaa jela mungu amemuandikia na akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi na Magereza Maranda aliamka kwenye kiti alichokuwa ameketi na kuwafuata wapiga picha na kuanza kukagua kamera ya mpiga picha mmoja kama endapo alikuwa amempiga picha na wakati akifanya hayo wanausalama hao walikuwa wakimwangalia  hali iliyosababisha wapiga picha hao kuingiwa na woga na kushindwa kumpiga picha akiwa ameketi ndani ya chumba cha mahakama.

Hukumu hiyo ya ilianza kusomewa jana saa 8 hadi saa 11:56 jioni na Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo Ilvin Mugeta kwaniaba ya wanajopo wenzie Jaji Samuel Karua na Beatrice Mutungi ambao walisema washitakiwa walikuwa wakikabiliwa na makosa sita ambayo ni kula njama kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kughushi jina la biashara la kampuni feki ya Lakshmil Textile  Mills Co Ltd ya India  na hati ya kuamisha deni iliyonyesha kampuni ya Maranda na Farijala ya Mibare Farm imepewa idhini ya kudai la kampuni hiyo ya India katika  BoT , kuwasilisha nyaraka zilizogushiwa katika Benki ya Afrika na Benki Kuu ambazo zilionyesha nyaraka hizo zilikuwa zimetolewa na BRELA,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kujipatia ingizo  toka BoT na kuisababishia BoT hasara ya Sh bilioni 3.8 ambapo kosa hilo la sita lilikuwa likiwakabili maofisa wa BoT ambao ni mshtakiwa wa 4,5 na 6 ambao ni (Iman Mwakosya, Ester Komu na Kaimu Katibu BoT,Sophia Lalika ambao walikuwa wakitetewa na Richard Rweyongeza na Majura Magafu na Ademba Agomba.

Hakimu Mugeta akiisoma hukumu hiyo alisema mahakama imefikia uamuzi wa kulifuta kosa la tano ambalo ni la kujipatia ingizo ambalo linamkabili mshtakiwa 1,2,3 ambao ni Farijala Hussein, Rajabu Maranda na Ajay Somai kwasababu upande wa jamhuri umefanya makosa ya kujumuisha kiwango cha fedha wanachowatuhumiwa kujipatia na kwamba mahakama imelifuta kosa hilo na pia imewaachilia huru washtakiwa wote katika kosa la kwanza la kula njama kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kosa hilo.

Hakimu Mugeta alisema hata hivyo upande wa Jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na wakili mwandamizi wa serikali Oswald Tibabyekomya, Shadrack Kimaro, Tumaini Kweka umeweza kuthibitisha shtaka la kughushi,kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kuwasilisha nyaraka zilizoghushiwa na kuisababishia serikali hasara na kwamba mashahidi wote saba na vielelezo vya  upande wa jamhuri vimeweza kuishawishi mahakama hiyo kuwatia hatiani kwa makosa hayo yaliyothibitishwa na upande wa jamhuri.

Alisema katika kosa la pili, mahakama hiyo imemtia hatiani Farijala peke yake na kwamba atatumikia adhabu kifungo cha jela miaka mitatu jela, kosa la tatu   ni Maranda na Farijala wametiwa hatiani na watatumikia adhabu ya miaka miwili jela,na kosa la nne mahakama imemtia hatiani Farijala, Maranda na Ajay Somai ambao watakwenda jela miaka miwili na kosa la sita ni la kusababisha hasara ambapo mahakam imewatia hatia maofisa hao wa BoT, Mwakosya, Komu na Lalika  ambapo watalipa faidi ya Sh.milioni tano kila mmoja na endapo watashindwa watakwenda jela miaka mitatu.

Aidha Hakimu Mugeta alisema mahakama yake imesikiliza ombi la wakili Mwandamizi wa serikali Kimaro ambaye alitaka mahakama hiyo iwaamuru washitakiwa warejeshe serikalini kiasi cha fedha ambacho serikali imepata hasara lakini imekubaliana na hoja wakili wa utetezi Majura Magafu ambayo ilidai kuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaonyesha maofisa wa BoT walinufaika na kiasi hicho cha fedha ila kuna ushahidi unaonyesha Maranda, farijala na Somai walinufaika na kiasi hicho cha fedha.

“Kwa sababu hiyo  mahakama hiyo inamwamuru Farijala kuilipa serikali fidia ya Sh 82,956,400, Maranda alipe Sh.616,443,600.10 na Somai alipe Sh milioni 400 na endapo watashindwa kuilipa serikali fidia hiyo basi mali zao zitakamatwa na kuongeza kuwa adhabu hiyo washtakiwa wataanza kuitumikia kuanzia jana’alisema Mugeta hukumu washtakiwa hao wakilekwa na machozi kizimbani.

Hii ni kesi ya tatu kati ya 11 za wizi wa fedha za EPA zilizofunguliwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Novemba 2008  zilizokwisha tolewa hukumu dhidi ya washtakiwa mbalimbali ,kutolewa hukumu.Hukumu kwanza ni kesi ya jinai Na.1161/2008 iliyokuwa ikimkabili Maranda na Farijala ya wizi wa sh bilioni 1.8 ambapo ilitolewa hukumu Mei mwaka jana, ambapo walikutwa na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na kesi nyingine ya EPA ni jinai Na. 1163/2008 ambapo Maranda na Farijala  Mei mwaka huu, walitiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kwenda jela miaka mitatu na hukumu nyingine ni kesi hii Na.1164/2008  ambayo ilitolewa hukumu jana na washtakiwa wakapatiakana na hatia.Kwa hiyo hivi sasa Maranda atabakia akikabiliwa na kesi nyingine mbili za EPA na Farijala atabakiwa akikabiliwa na kesi moja ya EPA ambazo bado hazijatolewa hukumu.

Baada ya Hakimu Mugeta kumaliza kutoa hukumu hiyo saa 11:56 jioni Mwakosyi,Komu na Lalika walishindwa kulipa kiasi cha fidia walichoamriwa na mahakama walipe hivyo wakaungana na Maranda na Farijala kwenda gerezani.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Novemba 23 mwaka 2012.

2 comments:

Anonymous said...

Τoԁay, I went to the beachfront with my kiԁs.

I found a seа ѕhell and gavе
it to my 4 year olԁ daughtеr and said "You can hear the ocean if you put this to your ear." Ѕhe placеd the ѕhell to
her ear and ѕcгeamed. There was a hermіt crab inside and it pinched her eаr.

She never wаnts to go bacκ! LoL I κnow this is entirely off topic but I had to tell someone!

http://wωw.discogs.сom/groups/topic/352280
Also visit my blog - Fun Size Movie Online

Anonymous said...

Нi there! Quіck questіοn that's entirely off topic. Do you know how to make your site mobile friendly? My weblog looks weird when browsing from my iphone. I'm trуіng to find a theme or plugin
that might be ablе tο resolvе this problem.
If you have anу suggeѕtiοnѕ, please share.
Thаnks!Wreck-It Ralph HD Free Streaming
Also see my web site :: Wreck-It Ralph HD Free Streaming

Powered by Blogger.