DPP ASHINDA RUFAA KESI YA RICHMOND
Na Happiness
Katabazi
MAHAKAMA Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, imeufuta uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar
es Saalam, uliomuona Mkurugenzi wa kampuni ya Richmond Ltd, Naeem Adam Gire aliyekuwa
akikabiliwa na makosa ya kughushi,kuwasilisha nyaraka za uongo na kutoa taarifa
za uongo kwa maofisa wa umma kuwa wana kesi ya kujibu.
Hukumu hiyo
ilitolewa kutoka na rufaa Na.126/2001 iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Eliezer
Feleshi dhidi ya uamuzi wa kesi ya kutoa
taarifa za uongo kwa Shirika la Umeme la Tanesco Na. 15/2009 iliyokuwa ikimkabili
Gire ambapo mwaka juzi Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alimuona hana kesi ya
kujibu.
Hukumu hiyo
ilitolewa na jaji Lawrance Kaduri ambaye katika hukumu yake hiyo amesema
asikiliza hoja za mawakili wa serikali waliokuwa wakimwakilisha mwomba rufaa (DPP), Fredrick Manyanda na
Oswald Tibabyekomya na mjibu rufaa alikuwa akiwakilishwa na wakili wa
kujitegemea Alex Mgongolwa.
‘Baada ya
kusikiliza hoja zote mbili na pia nimeangalia nakala ya uamuzi wa mahakama ya
kisutu uliomwachiria huru Gire kwa maelezo kuwa hana kesi ya kujibu, mahakama
hii imefikia uamuzi wa kuufuta uamuzi huo kwasababu imebaini kuwa kulikuwa na
ushahidi wa kutosha ulioletwa na upande wa jamhuri kule katika Mahakama ya
Kisutu ambapo umejitosheleza kumfanya Gire apande kizimbani na aanze kujitetea”alisema
Jaji Kaduri.
Jaji Kaduri
alisema anakubaliana na hoja za wakili wa Tibabyekomya iliyodai kuwa Hakimu
Lema alikosea kisheria katika uamuzi wake alisema kuwa kosa la kughushi
limeshindwa kuthibitika uamuzi ambao jaji huyo alisema hakimu Lema alisema
alitumia sheria ambayo ilishapitwa na wakati kwa kusema kosa la kughushi
limeshindwa kuthibitika.
‘Alisema
Gire anakabiliwa na kosa la kuwasilisha nyaraka za uongo hivyo ushahidi
unaonyesha Gire aliwasilisha
Alisema kwa mujibu wa hati ya mashitaka kosa
hilo la kughushi ,Gire anadaiwa kulitenda Machi 13 mwaka 2006 Dar es Salaam,
kwania ya ovu alighushi nguvu ya
kisheria(Power of Attoney)ya Machi 13 mwaka 2006 kwa lengo la kuonyesha Mohamed Gire
ambaye ni Mwenyekiti wa Kampuni
ya Richmond Development Company LLC ya Texa America amesaini hati ya
nguvu ya kisheria inayompa mamlaka Naeem Adam Gire (Mjibu Rufaa) wa hapa
jijijini kuendelea na shughuli za
kibiashara za kampuni hiyo hapa nchini kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha
335(d) (iii) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002.
“Hivyo basi
mahakama hii inakubaliana na mawakili wa mwomba rufaa(DPP), kuwa kosa hilo la
kughushi hati ya nguvu ya kisheria liliweza kuthibitishwa na upande wa jamhuri
hivyo mahakama hii inatamka wazi Hakimu Lema alikosea kisheria kusema upande wa
jamhuri ulishindwa kuthibitisha kosa la kughushia hati ya nguvu za kisheria na
kuwasilisha nyaraka hiyo hiyo ambayo ilighushiwa kwa maofisa wa umma kwa lengo
la kuonyesha kampuni hiyo ilikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme hapa nchini
wakati si kweli ili wapewe zabuni’alisema Jaji Kaduri.
Aidha Jaji
Kaduri alisema mahakama yake imejiridhisha kuwa kosa la kwanza na la
pili(Kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo) limeweza kuthibitishwa na upande
wa jamhuri, hivyo mahakama yake inaamuru kesi
ya msingi iliyokuwa imemalizika kwa Gire kuwaachiliwa huru baada ya
kuonekana hana kesi ya kujibu, irudi upya katika Mahakama ya Kisutu na Gire
anaanze kujitetea.
Mwaka juzi,
Hakimu Mkazi wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Waliandware Lema alimwachilia
huru Gire baada ya kumuona hana kesi ya kujibu na hakimu huyo alikwenda mbali
zaidi na kusema upande wa jamhuri uache kufungua kesi kwa kukurupuka na kwamba
mwisho wa siku mahakama inapowaachiria huru washitakiwa, matokeo yake mahakama inakuja
kubebeshwa lawama.
Chanzo:Gazeti la
Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 17 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment