KESI YA LWAKATARE YAIVA MAHAKAMANI
Na Happiness Katabazi
UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya tuhuma za ugaidi inayomkabili
Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema),
Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph,ulieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi
hiyo umekamilika.
Mbele ya Hakimu Mkazi Alocye Katemana, Wakili
Mwandamizi wa Serikali, Peter Mahugo alianza kwa kuikumbusha mahakama kuwa kesi
hiyo jana ilikuja kwaajili ya kutajwa na kwamba kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi
upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na hakimu Katemana aliiarisha kesi hiyo hadi
Mei 13 kwa ajili ya kutajwa na akaamuru
washitakiwa warejeshwe rmumande.
Machi 20 mwaka huu, ilidaiwa mawakili wa serikali waandamizi Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo,
kuwa kosa la kwanza ambalo linawakabii washitakiwa wote kuwa ni la
kula njama kutenda kosa la jinai kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002
, na kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o Stopover, wote kwa pamoja walitenda kosa hilo
kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la
kumdhuru Denis Msaki ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la
Mwananchi ambalo ni kinyume na kifungu cha 227 cha sheria hiyo.
Wakili
Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa
ni la kula njama ambalo pia ni kwaajili
ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na
kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo
washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la
kutaka kumteka Msaki kinyume na
kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya
Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.
Shitaka
la tatu ni la washitakiwa wote ambapo wanashitakiwa kwa kosa la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu cha 59(a) cha Sheria ya
Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki katika mkutano wa
kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki kinyume na kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria
ya Kuzuia Ugaidi.
Shitaka
la nne, Rweyongeza alidai linamkabili Lwakatare peke yake ni aliwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi
kinyume na kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28
mwaka jana, Lwakatale akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka
King’ong’o kwa makusudi aliliruhusu
kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka
nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka hayo.
Chanzo: www.katabazihappy.blosgpot.com;
Mei Mosi mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment