Header Ads

SHEIKH PONDA KUHUKUMIWA LEO MEI 9/2013







Na Happiness Katabazi

HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu Dar es  Salaam, Victoria Nongwa leo anatarajiwa kuketi katika kiti cha enzi na kutoa hukumu katika kesi ya uchochezi na wizi wa malighafi zenye thamani ya Sh.milioni 59 inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49.

Hukumu hiyo ambayo inasubiriwa kwa shahukumu kubwa na watu  inaratajiwa kutolewa leo kufuatia aprili 18 mwaka huu, mahakama hiyo kushindwa kutoa hukumu hiyo kwasababu hakimu Nongwa hakuwepo na hivyo kupanga tarehe ya leo kuwa ndiyo siku ya hukumu ya kesi hiyo itatolewa leo.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za kuaminika toka ndani ya Jeshi la Polisi ,vimeliambia gazeti hili kuwa vimejipanga kuimalisha ulinzi mkali leo ndani na nje ya mahakama ya Kisutu licha siku zote wa kesi hiyo wakati ikisikilizwa wanausalama waliimalisha ulinzi wa hali ya juu ukilinganisha na na ulinzi unaokuwepo wakati wa kesi nyingine zinapokuwa zikiendelea mahakamani hapo.

Aprili 3 mwaka huu:Mawakili wa upande wa Jamhuri ,Tumaini Kweka na Jessy Peter na mawakili wa utetezi Juma Nassor na Njama waliwasilisha majumuisho yao mahakamani hapo kwa njia ya maandishi ambapo mawakili wa upande wa jamhuri waliiomba mahakama iwaone washitakiwa wote wana hatia na wapewe adhabu kwa mujibu wa sheria.

Wakati mawakili wa utetezi waliiomba mahakama iwaone washitakiwa hawana hatia na iwaachilie huru kwa sababu hawakutenda  makosa yanayowakabili na kwamba upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi yao.

Machi 21 mwaka huu;Sheik Ponda, mshitakiwa wa tano Mukadamu Swaleh walijitetea.Na washitakiwa wenzake wa nne nao walijitetea siku hiyo na hivyo kufanya jumla ya washitakiwa 48 wa kesi hiyo kumaliza kutoa utetezi wao.Na siku hii ndipo upande wa utetezi walifunga utetezi wao na Hakimu Nongwa aliipanga tarehe ya jana ndiyo angetoa hukumu ya kesi hiyo.

Machi 4 mwaka huu:  Hakimu Nongwa atoa uamuzi wake ambapo aliwaona washitakiwa wote wana kesi ya kujibu na akatupilia mbali hoja ya mawakili wa utetezi iliyokuwa ikidai kesi hiyo ni ya madai na kwamba ifutwe.

Oktoba 18 mwaka jana, Ponda na wenzake walifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza ambapo wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka alidai washitakiwa hao wanakabiliwa na makosa matano na makosa hayo ni kama yafuatayo.

Shitaka la kwanza  kwanza ni la kula njama kinyume na kifungu 384 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2012,kwamba Oktoba 12 mwaka huu, huko eneo la Chang’ombe Markasi washitakiwa wote walikula  kwa nia ya kutenda kosa hilo.

Shitaka la pili wakili Kweka alidai linawakabili washitakiwa wote ambalo ni la kuingia kwa nguvu  kwa nia ya kutenda kosa  kinyume na kiufungu cha 85 na 35 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu  na kwamba  Oktoba 12 mwaka huu,  huko Chang’ombe  Markasi , kwa jinai  wasipokuwa na sababu  za msingi  washitakiwa hao waliingia  kwenye kiwanja kinachomilikiwa kampuni ya AgriTanzania  Ltd  kwania ya kujimilikisha  kiwanja hicho isivyo halali.

Kabla ya washitakiwa hakubali au kataa shitala hilo Ponda aliripoka na kusema yeye anakanusha shitaka hilo na kwamba washitakiwa wenzake nao wanalikanusha shitaka hilo,jambo ambalo lilikataliwa na Hakimu Sanga ambaye alimrisha kila mshitakiwa ajibu shitaka hilo kwa kinywa chake ambapo kila mshitakiwa kwa kinywa chake alikanusha shitaka hilo kinyume na alivyokuwa anataka Ponda iwe kwa yeye kukanusha shitaka hilo kwa niaba ya wenzake.

Wakili Kweka alilitaja shitaka la tatu kuwa ni  kujimilikisha  kiwanja kwa jinai kinyume na kifungu cha 86 na 35 cha sheria hiyo  na kwamba kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu huko Chang’ambe  Markasi  pasipo na uhalali wowote washitakiwa wote  katika hali  iliyokuwa ikipelekea  uvunjifu wa amani  walijimilikisha  kwa nguvu ardhi  ya  kampuni ya Agritanza Ltd.

Shitaka la nne, wakili Kweka alidai ni la wizi  ambalo ni kinyume na kifungu cha 258  cha sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002, na kuwa kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu,  washitakiwa hao waliiba vifaa na malighafi,matofali 1500,nondo,Tani 36 za Kokoto vitu vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh 59,650,000 mali ya kampuni ya Agritanza Ltd.

Aidha shitaka la tano Kweka alidai ni la uchochezi ambalo linamkabili Sheikh Ponda peke yake  ambalo ni kinyume na kifungu cha 390 na 35 cha sheria hiyo  kwamba kati ya Oktoba 12-16 mwaka huu katika eneo hilo la Chang’ombe Markasi  kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu(T) aliwashawishi  wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao  kutenda makosa hayo  na kwamba upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Mheshimiwa hakimu pamoja na kuwasomea mashitaka hayo ambayo yanadhamana kwa mujibu wa sheria, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), Dk.Elizer Feleshi kwa mkono wake amenituma kuwasilisha kwaniaba yake mahakamani hapo hati ya kufunga dhamana kwa mshitakiwa wa kwanza (Ponda) peke yake chini ya kifungu cha  148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2012’alidai wakili Kweka.

Na hakimu huyo alisema mahakama

yake imefungwa mkono kwasababu haiwezi kuipinga hati hiyo ya DPP na hivyo akaamuru Ponda na mshitakiwa wa tano kubaki rumande na washitakiwa wengine waliosalia walipata dhamana.Na tangu  Oktoba 18 mwaka jana hadi leo Ponda na Mkadamu walikuwa wakiishi gerezani kwasababu dhamana yao ilikuwa imefungwa na DPP.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Mei 9 mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.