JOSEPH MUSHUMBUSI SI MKE WA MAIMBO-MAHAKAMA
Na Happiness Katabazi
HATIMAYE
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, imetupilia mbali rufaa iliyokuwa
imekatwa na aliyekuwa mume wa Josephine Mushumbusi, Maimbo baada ya
kuiona rufaa hiyo haina msingi wowote kisheria.
Hukumu hiyo ya rufaa ya madai
ya ndoa Na.32/2012 ilitolewa jana na Hakimu Aniseth Wambura ambapo
alisema mahakama yake imefikia uamuzi huo wa kuitupa rufaa hiyo
kwasababu haina mantiki ya kisheria.
Hakimu
Wambura alisema mahakama yake imekubalina na hukumu iliyotolewa Aprili
2012 na Mahakama ya Mwanzo Sinza katika kesi ya madai talaka iliyokuwa
imefunguliwa na Mushumbusi anayetetewa na wakili wa kujitegemea Philemon
Mutakyamilwa dhidi ya Maimbo ambapo mahakama
hiyo ya chini ilitangaza kuwa hakukuwa na ndoa baina ya watu hao
kwasababu Maimbo alikuwa ni mzinzi, simwaminifu katika ndoa yake na
alikuwa akimtesa mkewe.
“Baada
ya mahakama yangu kusikiliza hoja za mwomba rufaa na mjibu rufaa
,mahakama hii imefikia uamuzi wa kukubali hoja za Mushumbisi kuwa kwa
tabia ile ya mbaya ya uzinzi na ukosefu wa uaminifu katika ndoa yake
hapakuwepo na ndoa baina yao hivyo mahakama yake inatangaza kuwa hukumu
ya mahakama ya Mwanzo Sinza ambayo iliivunja ndoa hiyo ilikuwa hukumu
sahihi “alisema hakimu Wambura.
Akizungumza
na gazeti hili baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili Mutakyamilwa
alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwani mahakama imetenda haki kwasababu
kesi hiyo ya madai ya talaka ilikuwa na msukumo wa siasa chafu
zilizokuwa na lengo chafu la kumchafulia jina mteja wake(Mshumbusi)
ambaye kwa sasa ni mzazi mwenzie Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Dk.Wilbroad Slaa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Mei 24 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment