MENEJA BENKI YA ACCESS KORTINI KWA WIZI
Na Happiness Katabazi
MENEJA
wa Benki Access, Fadhil Muzo na maofisa wa mikopo wa benki hiyo
wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam,
wakikabiliwa na makosa ya wizi na uharibifu wa mali zenye thamani ya
zaidi ya Sh.milioni 45,246,600.
Wakili wa Serikali Hilda Kato mbele ya Hakimu Mkazi Aniseth Wambura alidai kuwa mbali ya Muzo washitakiwa wengine ni Michael Ntinga,Luka Tumbuka ambao ni maofisa mikopo na Issack Nchembi ambaye ni dereva na kwamba wote wanakabiliwa na jumla ya makosa matatu.
Wakili Kato alilitaja kosa la kwanza kuwa ni la kula njama, kosa la pili ni la wizi ambalo walilitenda Januari 29 mwaka huu, katika eneo la Manzese jijini ambao waliiba bidhaa mbalimbali ikiwemo kreti za soda 31,katoni moja ya soda, katoni 53 za maji ya uhai, kreti 11
za bia aina ya Serengeti,katoni nne za bia aina ya Tusker, zenye jumla
ya thamani ya Sh 45,246,600 mnali ya Rahamat Rashid Mandali.
Wakili
Kato alilitaja kosa la tatu kuwa ni la uharibu wa mali ambalo
walilitenda Januarui 29 mwaka huu, huko Manzese ambapo waliaribu Mlango
wa ‘Gril’ wenye thamani y ash 250,000, mlango wa mbao wenye thamani ya
Sh.90,000 na vishikizo vya kushikia mlango huo vitu vyote hivyo vina
thamani ya Sh. 420,500 mali ya Wilbert Makishe.
Na
wakili Kato alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba
wanaomba mahakama iwapangie tarehe ya kuja kuwasomea maelezo ya awali.
Hata
hivyo washitakiwa hao walikana mashitaka na walitimiza masharti ya
dhamana yaliyomtaka kila mshitakiwa asaini bondi ya Sh.milioni nne.
Kwa
upande wake Hakimu Wambura aliairisha kesi hiyo Juni 24 mwaka huu, kesi
hiyo itakapokuja kwaajili ya upande wa jamhuri kuwasomea maelezo ya
awali washitakiwa.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumatano, Mei 29 mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment