Header Ads

MAHAKAMA INAUHABA WA WASAJILI


Na Happiness Katabazi

JAJI Kiongozi wa Mahakama Kuu nchini, Fakhi Jundu amesema kuwa bado mhimili wa mahakama unakabiliwa uhaba wa wasajili wa mahakama.

Jaji Jundu aliyasema hayo jana katika sherehe za kumuapisha Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba, Charles Maximilian Magesa zilizofanyika katika Mahakama Kuu Kanda ya  Dar es Salaam.

Jaji Jundu alisema kwa sasa Mahakama Kuu  nchini ina jumla ya wasajili wa wilaya 40, idadi ambayo alisema ni ndogo ambapo ili kukabiliana na tatizo hilo la uhaba ,mhimili huo unaitaji kupata nusu ya  idadi nyingine kama hiyo ili huduma zinazotakiwa kutolewa kwa wananchi kupitia wasajili ziweze kutolewa kwa wananchi wote wanazoziitaji.

Jaji Jundu alisema Msajili ni mtu mhimu sana kwani msajili wa mahakama ni mtu ambaye anashughulika na kesi zote zinazofunguliwa na kuendeshwa katika mahakama husika na anayefahamu ratibu za kesi hizo na ndiye anashughulika na masuala ya mahakama katika ngazi mbalimbali.

“Sasa hivi mhimili wa mahakama unakabiliwa na uhaba wa wasajili na hadi sasa mahakama ina jumla ya wasajili 40  na katika kutekeleza azma ya mahakama ya kutenganisha shughuli za kimahakama na shughuli za kiutalawa ,mhimili huo  unaitaji  kupata nusu  ya idadi hiyo ya wasajili  ili azima yao iweze kutekelezwa na kwamba azma ya mahakama ni kuwa na Mahakama Kuu  kila Mkoa  kwahiyo wasajili waliopo ni wachache”alisema Jaji Jundu.
Kwa upande wake Msajili Magesa alisema kwanza anafurahi kwa kupata wadhifa huo na kwamba aqnafahamu mhimili wa mahakama unakabiliwa na  changamoto za miundombinu,watumishi wachache na majengo yasiyokidhi lakini yeye ataakikisha  wananchi wanaofika mahakamani kutafuta huduma wanapa huduma kwa wakati .

Magesa alisema kwani kuna baadhi ya wananchi wanaonekana kukata tamaa na kuanza kujichukulia sheria mkononi lakini yye anaamini kuwa kama haki itakuwa inatolewa kwa wahusika kwa wakati ,itaepusha hali hiyo ya wananchi kujichukulia sheria mkononi na kukata tamaa na kuongeza kuwa ataakikisha  watumishi wa mahakama  wanatoa huduma na haki kwa wananchi wanaofika mahakamani kuitaji huduma za kimahakama.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Mei 11 mwaka 2013.

No comments:

Powered by Blogger.