NAENDELEA KUMLILIA WAKILI STANSLAUS BONIFACE 'JEMBE'
Na Happiness Katabazi
Leo Mei 27 mwaka 2013, mpendwa wetu aliyekuwa Wakili Kiongozi wa Serikali
mwenye cheo cha Mkurugenzi Msaidizi wa ofisi ya
Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, Stanslaus Boniface Makulilo (44) ‘Jembe’
afariki ghafla tarehe kama ya leo
katika Hospitali ya Regency jijini Dar
es Salaam.
Binafsi mimi
na wengine wote tunaoheshimu mchango wako wa Taaluma ya sheria uliyokuwa
ukiiutoa kwenye mashauri mbalimbali yaliyokuwa yakiendeshwa katika mahakama
mbalimbali hapa nchini, na wale mawakili wa serikali uliokuwa ukiwafundisha
kazi tunaendelea kukumbuka na kukuenzi.
Na ndiyo
maana leo hii mimi binafsi nikiwa Mwandishi wa Habari za Mahakamani na
mwanafunzi wa mwaka wa pili wa fani ya
Sheria,ndiyo maana nimechukua muda wangu na
na ndiyo maana hata leo hii nimeweza kuchukua muda wangu na kuketi
kitako na kuandika makala hii ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo chako, na kukusimulia
ni kesi gani za jinai kubwa zilifunguliwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini
DPP-Dk.Eliezer Feleshi na vijana wako uliowafundisha kazi waliweza kuziendesha
kikamilifu na wakafanikiwa kushinda na nyingine wakashindwa na kesi nyingine ulizoziacha
nyingine zimeishatolewa hukumu na nyingine bado.
Nianze kwa
kukusimulia kesi kubwa kufunguliwa baada yaw ewe kufariki ni kesi ya uhujumu
uchumi na madai ya kupokea rushwa inayomkabili Waziri wazamani Idd Simba na
wenzake.Kesi hii ilifunguliwa rasmi siku
ambayo wewe Boniface ulikuwa unazikwa pale katika Makaburi ya Kinondoni na ilikuwa ni Mei 29 mwaka jana, na hadi sasa
bado haijaanza kusikilizwa.
Lakini pia
Oktoba 18 mwaka jana, Dpp alimfungulia kesi wizi wa malighafi za Sh.milioni 59
na uchochezi Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Shaikh Ponda Issa Ponda
na wenzake 49. Na DPP aliwasilisha hati ya kumfungia dhamana Ponda na Mkadamu
Abdalah na kweli walisota gerezani hadi kesi hiyo ilipotolewa hukumu Mei 9
mwaka huu, ambapo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Victoria
Nongwa alimpotia hatiani Ponda peke yake kwa kosa moja la kuingia kwa jiani
katika kiwanja cha Markazi Chang’ombe na kuwaachiria washitakiwa wengine 49 kwa
maelezo kuwa jamhuri imeshindwa kuthibitisha kesi dhidi yao na hivyo Hakimu
Nongwa akaamuru Ponda kutumikia adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja nje.
Kwa upande
wa jamhuri katika kesi hii ulikuwa ukiwakilishwa na wakili mwandamizi wa
serikali Tumaini Kweka ambaye kwasasa ni wazi amekuwa akitajwa tajwa na watu
wanaomshuhudia wakati akiendesha mashauri mbalimbali ya jinai, kuwa anafuata
nyayo za marehemu Boniface.
Kesi
nyingine ni kesi ya wafusi 53 wa Sheikh Ponda ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa
Hakimu Mkazi Sundi Fimbo, ambapo Machi
21 mwaka huu, alitoa hukumu ya kuwafunga mwaka mmoja jela baada ya kuwatia
hatiani kwa makosa ya kufanya mkusanyiko haramu na kukaidi amri ya jeshi la
polisi iliyowataka watawanyike na wasiandamane kwenda ofisi ya DPP, kumshinika
ampatie Ponda dhamana.
Lakini pia Machi 20 mwaka huu, Jamhuri
ilimfungulia kesi ya tuhama za ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph lakini hata hivyo Lwakatare alikimbilia
Mahakama Kuu kuomba mahakama hiyo iitishe jalada la kesi hiyo na ilipitie kuona
kama DPP alikuwa sahihi kumfungulia mashitaka Lwakatare ya ugaidi Machi 18 na
kisha Machi 20 asubuhi kuyafuta na kisha Machi 20 mchana kumfungulia tena kesi
yenye makosa hay ohayo ambapo Jaji
Lawrence Kaduri katika uamuzi wake aliotuoa Mei 8 mwaka huu, alimfutia
mashitaka matatu ya ugaidi Lwakatare na kumbakizia kosa moja la kula njama
kutaka kumuua kwa sumu Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mwananchi Denis Msacky.
Lakini hata
hivyo Mei 8 mwaka huu, Jaji Kaduri alitoa uamuzi wa maombi hayo ya Lwakatare
ambapo alisema DPP alikuwa sahihi kufuta na kumfulia mashitaka hayo, ila jaji
huyo pia akatoa uamuzi wa kumfutia jumla ya makosa matatu ya ugaidi.
Hata hivyo
Mei 21 mwaka huu, DPP aliwasilisha ombi lake Mahakama ya Rufani nchini akiomba
mahakama hiyo itengue uamuzi huo wa mahakama kuu wa kumfutia Lwakatare mashitaka ya ugaidi na hadi sasa bado uongozi
wa mahakama ya rufaa haujapanga tarehe wala majaji wa kuanza kusikiliza rufaa
hiyo.Na kesi ya msingi ya Lwakatare inakuja leo katika mahakama ya Kisutu
kwaajili ya kutajwa mbele ya hakimu Mkazi Alocye Katemana.Na tangu Machi 18
mwaka huu hadi leo Lwakatare bado wapo katika gereza la Segerea kwasababu kesi
inayowakabili haina dhamana.
Lakini hata
hivyo Boniface Mei mwaka huu, Jaji wa Mahakama Kuu, Dk.Faudhi Twaibu alitoa
amri ya kutupilia mbali hoja za mawakili wa jamhuri uliokuwa ukiwakilishwa na
Oswald Tibabyekomya katika ile rufaa yetu ya kupinga hukumu ya kesi ya madai ya
kuomba rushwa iliyokuwa ikimkabili Jerry Murro ambapo upande wa jamhuri ulikuwa
ukiomba mahakama hiyo itoe amri ya kesi hiyo ilirudishwe mahakama ya Kisutu
ianze upya kwasababu mwenendo wa kesi hiyo hausomeki vizuri, lakini Jaji Twaib
alisema anatupilia mbali ombi hilo na kwamba sababu za kufikia uamuzi huo
ameziifadhi.
Pia wakili Boniface Aprili mwaka huu, Jaji
Kaduri wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, alikubali rufaa iliyokuwa
imekatwa na DPP katika kesi ya kupinga uamuzi wa Hakimu MKazi wa Mahakama ya
Hakimu mkazi Kisutu,Waliarwande Lema ambapo ulimuona Kigogo wa Kampuni ya
Richmond Naeem Gire hana kesi ya kujibu.
Jaji Kaduri katika hukumu yake hiyo
alisema kulikuwa na ushahidi wa kutosha ambao unamfanya Gire apande kizimbani
ajitetea na hivyo hakimu Lema alikosea na hivyo jaji huyo akaamuru Gire apande
katika mahakama ya Kisutu naanze kujitetea na tayari uongozi wa mahakama ya
Hakimu mkazi Kisutu umeishampangia hakimu Emilius
Mchauru kuanza kusikiliza
utetezi wa Gire Juni 6 mwaka huu.
Lakini hata
hivyo tayari Gire ameishawasilisha hati ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama
Kuu na kwamba anachosubiri ni uogozi wa mahakama kuu umpatie nakala ya hukumu
hiyo ili aweze kuandaa hoja zake na kuziwasilisha katika mahakama ya rufaa ni
nchini kupinga hukumu hiyo.
Kuhusu zile
jumla ya kesi 11 za wizi katika akaunti za EPA katika Benki Kuu, ambazo wewe na
mawakili wenzako mlikuwa mkiziendesha na hadi unakutwa na mauti uliweza
kufanikiwa kushuhudia kesi moja ya EPA ya wizi wa sh.bilioni 1.3 iliyokuwa
ikimkabili Rajabu Maranda na Farijala Hussein wakihukumiwa kwenda jela miaka
mitano, na ulivyofariki pia tayari kuna hukumu za kesi mbili za EPA ambazo
zinamhusisha Maranda ,Farijala na maofisa wa BOT watatu zilitolewa hukumu.
Hivyo kesi nyingine za EPA zilizosalia bado haizajatolewa hukumu .
Ila zile
kesi nne za EPA zinazomkabili mfanyabiashara maarufu Jeetu Patel zilizofunguliwa Novemba 2008 bado hata
shahidi mmoja wa upande wa jamhuri hawajaanza kupanda kizimbani kuanza kutosha
ushahidi wake.
Hizo ni
simulizi chache za baadhi ya kesi zilizovuta hisia katika jamii na sisi
waandishi wa habari kwa kipindi hiki cha mwaka mmoja ambacho wewe haupo nasi
duniani.Ila napenda nikuakikishie tu kuwa mawakili wa serikali bado wanatupatia
ushirikiano wa kutosha sisi waandishi wa habari za mahakamani kama zamani.
Unakumbukwa
na waandishi wa habari za mahakamani wenzangu Furaha Omary, Regina Kumba, Magai
James, Tausi Ally, Faustine Kapama, Kulwa Mzee,Grace Gurisha, Frola Mwakasala ,Karama
,Hellen Mwango.
Lakini bado
unakumbukwa na mawakili wenzako wa Serikali, Dk.Eliezer Feleshi, Biswalo
Mganga, Malangwe Mchungahela, Sedekia Emphere,Fredrick Manyanda,Oswald
Tibabyekomya, Lasdslaus Komanya, Tumaini Kweka, Ponsian Lukosi,Ben Lincoln,Arafa
Msafiri, Timon Vitalis,Michael Lwena na wengine wengi.Ambao kwa kadri ya uwezo
wao wafanya vizuri katika majukumu yao ya ueneshaji wa mashitaka, na wengi
niliozungumza nao wanakushukuru kwa mchango wako wa kitaaluma kwani hukuwa
mchoyo wa kuwafundisha kazi pale walipoitaji msaada huo.
Miongoni mwa
kesi kubwa ambazo mimi binafsi nilimshuhudia Marehemu Boniface akiziendesha kwa zaidi ya miaka mitano katika
mahakama mbalimbali hapa nchini sasa ni kesi ya wizi wa shilingi bilioni 1.8
katika EPA, iliyokuwa ikimkabili Kada wa CCM, Rajabu Maranda na Farijala
Hussein ambapo mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Mei 23 mwaka juzi, iliwahukumu
kwenda jela miaka mitano, kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi
milioni 10 iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji
la TBC, Jerry Murro na wenzake ambapo Murro alishinda kesi hiyo mwaka juzi.
Kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mfanyabishara
Jayankumar Patel “Jeetu Patel’ na wenzake dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, DPP na Reginal Mengi iliyokuwa akitaka afutiwe kesi zake nne za EPA
zilizopo katika mahakama ya Kisutu kwasababu Mengi alimuhukumu kabla ya
hajahukumiwa na mahakama kwa sababu alimuita ni Fisadi Papa, ambapo Boniface
alimwakilisha AG na DPP na aliibuka mshindi katika kesi hiyo.
Kesi nyingine kubwa ambayo marehemu alikuwa
akiziendesha ambazo bado hadi umauti unamkuta hazijatolewa hukumu ni ile ya
mauji ya Ubungo Mataa ambayo inaendelewa kusikilizwa na Jaji Projestus Rugazia,
rufaa ya kupinga hukumu ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyomwona
mfanyabiashara Naeem Gile ambayo inasikilizwa mbele ya Jaji Laurence Kaduri
ambaye alikuwa akikabiliwa na makosa ya kutoa taarifa za uongo kuhusu kampuni
ya kufua umeme ya Richmond LCC, kuwa hana kesi ya kujibu, rufaa ya kupinga
hukumu ya mahakama ya Kisutu iliyomuona Jerry Murro hana hatia na kesi ya
matumizi mabaya na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7
inayomkabili waliokuwa mawaziri wa Fedha na Nishati, Basil Mramba, Daniel Yona
na Gray Mgonja ambapo kesi hii hivi sasa imefikia hatua ya Mramba kuendelea
kujitetea
Boniface
alizaliwa Februali 21 mwaka 1968 ameacha mke na watoto watatu, aliitimu shahaha
ya kwanza ya Sheria mwaka 1995 na shahada ya pili ya sheria alimaliza mwaka
2008 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Julai Mosi mwaka 1995 aliajiriwa
rasmi katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali kama Wakili wa Serikali, ilipofika
Oktoba Mosi mwaka 2006 alipandishwa cheo na kuwa Wakili wa Serikali
Mwandamizi.Oktoba Mosi mwaka 2007 alipandishwa cheo tena na kuwa Wakili
Kiongozi wa Serikali.
Nyadhifa ambazo Boniface aliwahi kuzishika enzi za uhai
wake ni kati ya mwaka 2003-2007 alikuwa ni Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa
Mbeya.Kati ya Mei 2007 na Oktoba 2010 alikuwa Wakili wa Serikali Mfawidhi Kanda
ya Mwanza.Novemba 2009 hadi Novemba 2010 alikuwa Mwanasheria Mfawidhi wa
Serikali mkoani Dar es Salaam. Kutokana na utendaji kazi wake mzuri ilipofika
Desemba 2010 hadi mauti yanamkuta aliteuliwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi
Msaidizi wa Kitengo cha uendesha mashitaka na pia awaka Msimamizi wa uendeshaji
kesi zenye maslahi kwa umma. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake liimidiwe.
Leo
umetimiza mwaka mmoja tangu Boniface ufariki dunia, naendelea kukulia.
Chanzo:www.katabazihappy.blogspot.com
Facebook:happy
katabazi ; Jumatatu, Mei 27 mwaka 2013
0716 774494
No comments:
Post a Comment