Header Ads

JERRY MURRO ANA HATIA-SERIKALI



Na Happiness Katabazi

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya kula njama na kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 inayomkabili aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la (TBC1), Jerry Murro na wenzake imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam,imtie hatiani kwa kesi inayomkabili.



Ombi hilo liliwasilishwa jana kwa njia ya maandishi na Mkurugenzi Msaidizi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka, Stanslaus Boniface ikiwa ni utetekelezaji wa amri ya Hakimu Mkazi Frank Moshi aliyoitoa Oktoba 4 mwaka huu, ambapo alizitaka pande hizo mbili kuwasilisha majumuisho yao ya kuwaona washtakiwa wana hatia au la.Ambapo upande wa utetezi uliwasilisha majumuisho yao Oktoba 28 mwaka huu.

Siku hiyo ya Oktoba 4 mwaka huu, upande wa utetezi ulifunga ushahidi wao baada ya mshtakiwa wa pili na watatu na shahahidi wa shahidi wa kwanza walitoa ushahidi wao na walimaliza siku hiyo hiyo.

Boniface ambaye ni Wakili Kiongozi wa Serikali katika majumuisho yake ambayo nakala yake tunayo, anadai kwa mujibu wa mashahidi wa upande wa Jamhuri na utetezi uliotolewa na washtakiwa umethibitisha bila kuacha mashaka kuwa washtakiwa walitenda makosa ya kula njama, kuomba rushwa na kujifanya ni watumishi wa serikali.

Boniface alidai hoja ya Wakili wa Murro, Richard Rweyongeza inayodai kuwa Murro hakutenda makosa hayo na kwamba anashangaa ni kwanini polisi walifanya haraka kumkamata Murro wakati alikuwa hajapokea kiasi hicho cha fedha,ni dhahifu kwasabu kabla ya Murro kukakamatwa tayari aliyekuwa Mhasibu wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Michael Kalo Wage alishafika kituo cha polisi na kutoa taarifa kuwa mshtakiwa huyo amemwomba rushwa.

“Na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 kinasema kitendo cha kuomba rushwa ni kosa chini ya kifungu hicho ….sasa namshangaa sana wakili Rweyongeza anavyo dai ni kwanini polisi wasingesubiri Murro apokee zile Sh milioni 10 za rushwa.Tunaiomba mahakama iipuuze hoja hiyo ya wakili Rweyongeza kwasababu haina msingi kwani sheria hiyo ya kuzuia rushwa inatamka bayana mtu yoyote atayeomba rushwa, kupokea rushwa, kula njama ni makosa matatu yanayojitegemea na kitendo cha Murro kuomba rushwa tayari alikuwa ameishatenda kosa na ndiyo maana polisi walimkamata”alidai wakili Kiongozi wa Serikali Boniface.

Aidha Wakili Boniface aliomba mahakama hiyo iikate hoja wakili wa Murro iliyokuwa ikidai kuwa Murro alikamatwa katika Hoteli ya City Garden Februali mwaka jana wakati mshatiwa huyo hotelini hapo kwaajili ya kuudhulia mkutano nma waandishi wa habari, hoja ambayo wakili hiyo wa seriakali ni ya uongo kwani siku hiyo hapakuwepo na mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika hapo na ndiyo maana si Murro wala wakili wake Rweyongeza wameweza kuleta ushahahidi unaonyesha siku hiyo hotelini hapo ulifanyika mkutano na waandishi wa habari na pia wameshindwa kumleta mtu aliyekuwa ameuitisha mkutano huo ili aje kuidhibitishia mahakama kuwa alikuwa ameitisha mkutano siku hiyo na kwamba ni yeye ndiye alikuwa amempigia simu Murro ili aje hotelini hapo kuudhulia mkutano.

“Ni rai ya upande wa Jamhuri kuwa tumeweza kuithibitisha kesi yetu na tunaiomba mahakama imuone Murro na wenzake wana hatia katika kesi hii inayowakabili kwani ushahidi, vielelezo na utetezi waliotuoa mahakamani hapa umedhibitisha kuwa washtakiwa hao walitenda makosa yanayowakabili hivyo tunaiomba mahakama hii tukufu iwatie hatiani”alidai Wakili Boniface.

Kesi hiyo itakuja tena Oktoba 31 mwaka huu, kwaajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kutolewa hukumu.

Novemba 14 mwaka huu, washtakiwa hao walifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa ya kula njama, kuomba rushwa na kujifanya maofisa wa serikali ambapo walimuomba rushwa ya shilingi milioni 10 , Mhasibu wa Halmashauri ya Bagamayo ,Michael Wage ili Murro asiweze kurusha tuhuma za ufisadi zinazomkabili katika kipindi cha Usiku wa Habari kinachorushwa na Televisheni ya TBC1.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumamosi, Oktoba 29 mwaka 2011.

No comments:

Powered by Blogger.