KESI YA KUPINGA ADHABU YA KIFO YAANZA KUUNGURUMA
Na Happiness Katabazi
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeuamuru upande wa serikali katika kesi ya Kikatiba ya kupinga adhabu ya kifo kuwa ifikapo April 21 wawe wamejibu hoja za mawakili wa walalamikaji.
Walalamikaji katika kesi hiyo ni Tanganyika Law Society, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHCR),Sahringon-Tanzania Chapter dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambao wanatetewa na wakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa,Chacha Boke,Fulgence Massawe na Julius Rugazia.
Amri hiyo ilitolewa na jopo la majaji watatu waliokuwa wakiongozwa na Jaji Robert Makaramba,Razia Sheikh na Projest Rugazia walifikia kutoa uamuzi huo baada ya mwanasheria wa serikali Methew Mwaimu kuonyesha nia ya kujibu maombi ya mawakili hao.
Jaji Makaramba alisema anaairisha kesi hiyo hadi April 24 mwaka huu, kwaajili ya kutajwa. Kwa mujibu wa hati ya madai ya msingi, walalamikaji wanaiomba mahakama itamke kuwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa inavunja ibara 4(2),12(2),13(1),13(6)a,d,e,14,26(2),64(5) na 107(a) za Katiba ya nchi. Kwa vile utekelezaji wake ni wakikatili na kudhalilisha utu wa binadamu.
Aidha wanadai sheria husika ya adhafu ya kifo inalazimisha mahakama inapomkuta mtu ana hatia ni lazima anyongwe na kwamba haitoi adhabu mbadala kwa mahakama.Wakati Katiba ya nchi imetamka wazi kwamba kazi ya utoaji haki na adhabu zake ni kazi ya mahakama.
Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi,April 2 mwaka 2009

No comments:
Post a Comment