Header Ads

MHASIBU WA TRA KORTINI KWA UDANGANYIFU

Na Happiness Katabazi


MHASIBU wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Sangu John alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jana na kusomewa mashitaka 132 akidaiwa kujipatia zaidi ya Sh milioni 944 mali ya mwajiri wake kwa njia za udanganyifu pamoja na kulipa mishahara hewa.


Mashitaka hayo aliyosomewa mbele ya Hakimu Aloyce Katemana na mawakili kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ben Lincon, Osward Tibabyekomya wakisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro. Mashitaka yalikuwa ni ya kutumia nyaraka za uongo kumdanganya mwajiri wake, kughushi, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu na kusababisha hasara kwa mamlaka hiyo Sh 944,169,330.

Shitaka la kwanza alidaiwa June 19, 2006 katika ofisi za TRA makao makuu yaliyoko wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam kwa nia ya kudanganya alighushi orodha ya malipo ya mshahara kwa mwezi huo, akionyesha wafanyakazi hewa tisa wa shirika hilo walitakiwa walipwe Sh 12,000,000 akijua si kweli.

Katika mashitaka ya kutumia nyaraka kumpotosha mkuu wake wa kazi, alidaiwa moja wapo alidaiwa June 20, 2006 ofisi za TRA akiwa mwajiriwa aliwasilisha orodha hiyo kwa mkuu wake wa kazi akidai kwamba wafanyakazi hao walitakiwa kulipwa fedha hizo huku akijua sio kweli.

Mashitaka mengine alidaiwa kwa nia ya kudanganya alijipatia kutoka benki ya NBC fedha hizo akijidai kuwalipa watu hao kwa mshahara wa mwezi June 2006.
Katika mashitaka mengine alidaiwa kudai malipo hayo hewa miezi mingine kuanzia June 2006 hadi Augost 2009.

Mashitaka mengine John alidaiwa alighushi nyaraka kuonyesha mishahara ya wafanyakazi wa TRA mwezi Novemba ni Sh 2,207,122,430 akijua sio kweli, alidaiwa kuendelea kumdanganya mwajiri wake katika miezi mingine katika kipindi hicho akionyesha mishahara tofauti na iliyokuwa ikistahili wafanyakazi wa TRA kwa mwezi.

Aidha mshitakiwa huyo alishitakiwa pia kwa kufanya mchezo huo aliisababishia hasara mamlaka ya Mapato Tanzania ambayo ndio ilikuwa mwajiri wake Sh 944,169,330.

John alikana mashitaka yote na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kutoa nusu ya fedha hiyo ambayo ni Sh 472,084,665. Kesi hiyo imepangwa kutajwa Desemba 5 mwaka huu na upelelezi haujakamilika.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi, Novemba 24 mwaka 2011.

3 comments:

Jigambe Team said...

Hii ndo tanzania inayotakiwa...! from jigambeads.com

Anonymous said...

🌹 Ushuhuda Wangu Kuhusu Dkt. Dawn – Mtu Aliyerejesha Nyumba Yangu na Furaha Yangu

Nataka kushiriki ushuhuda wangu wa dhati kuhusu jinsi Dkt. Dawn alivyobadilisha maisha yangu kabisa.

Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na alikuwa ameenda kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwangu — na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

Lakini si hayo tu — Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyokuwa ikizunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote — huzuni, bahati mbaya, au mkanganyiko — usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com

Anonymous said...

Ushuhuda

Nilivunjika moyo kabisa uhusiano wangu ulipoisha. Niliamini kweli kwamba nilikuwa nimepoteza mpenzi wa maisha yangu milele. Kisha nikampata Dkt. Dawn, na kila kitu kikabadilika.
Kwa wema, hekima, na mwongozo wenye nguvu, alirudisha upendo niliodhani ulikuwa umetoweka. Leo, tuna furaha zaidi kuliko hapo awali!
Dkt. Dawn aligeuza machozi yangu kuwa furaha kweli.

Dkt. Dawn Anaweza Kukusaidia Kwa:

✅ Uchawi wa Mapenzi
✅ Uchawi wa Mimba
✅ Kurejesha Ndoa / Uhusiano
✅ Tiba za Mimea kwa VVU, Ugonjwa wa Figo, Matatizo ya Moyo, Maambukizi, na zaidi

📧 Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com
📞 Simu/WhatsApp: +2349046229159

Usiteseke kimya kimya. Dkt. Dawn anaweza kurudisha furaha maishani mwako!

Powered by Blogger.